WAKRISTO NA SIKU ZAO ZA IBADA SURA YA KWANZA

SURA YA KWANZA.
Ndiyo, kufanya ibada, ni kila siku, lakini si siku zote Mungu alizitakasa. Siku ya Sabato Pekee ndiyo Mungu aliitakasa na kuiweka wakfu kwa ajili ya wanadamu Marko 2:26-7. Angalia Mwanzo wa siku hiyo.
Sabato ilianza lini???
“Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya”
. (Mwanzo 2:2-3)

Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa Bwana; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi…                                                                                                                                    ( Kutoka 16: 23)
Muhimu: Sabato ilikuwepo hata kabla ya Amri 10 kutolewa pale Sinai. Wana wa Israeli waliitunza Sabato Waisraeli walizitunza Amri za Mungu kama Babu yao Ibrahimu. Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu. ( Mwz 26:5)
Kwa nini Mungu alifanya Sabato??
Sabato ni pumziko
Ishara ya Uumbaji
Sabato ni muhuri wa Mungu
Humtambulisha kuwa Mungu ni muumbaji wa vyote
Aliitenga kwa ajili ya mwanadamu ili mwanadamu aweze kuwasiliana na Mungu kila wiki
Mungu aliifanya kuwa tofauti (aliitakasa) na siku zingine zote sita
Jumapili haijatakaswa na Mungu, naam, hata kwenye Agano Jipya
Sabato ni siku ya furaha
Ajabu zaidi, Sabato ilianzishwa hata KABLA YA DHAMBI duniani,
iweje ikomeshwe msalabani au kubadilishwa.
        Hata baada ya taifa la Israel kupelekwa utumwani Misri kwa muda miaka 400, Mungu aliamua kuwatoa Waisrael utumwani kwa maana walikuwa wameshasahau kumwabudu Mungu na kugeukia miungu ya Misri. Wakiwa njiani, Mungu aliwataka wakumbuke na kumwabudu Mungu kama Baba zao walivyofanya hapo zamani. Ndiyo maana Mungu hakuanza na tunzeni sabato yangu, bali Ikumbuke…

”Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.”
(Kutoka 20:8-11)

Zingatia yafuatayo:-
Ni siku iliyokuwepo tangu uumbaji na itadumu milele maana ni agano lake na watu wake. “Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele.”                                                                                                                                 ( Kutoka 31:16)

Ni siku inayomtambulisha Mungu kuwa yeye ni muumbaji wa mbingu, nchi na vyote vilivyomo. “Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.”                                                      (Kutoka 20:11)

Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato kwa Bwana katika makao yenu yote.
         ( Mambo ya Walawi 23:3)

Ni ishara kati yake na watu wake (Sabato ni utambulisho wa watu wa Mungu). “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.”
(Ezekieli 20:12)

“Zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”                                                                                                                                 (Ezekieli 20:20)

Ni amri 4, Mungu ameaza na neno IKUMBUKE, maana waisrael waliisahau na Mungu alifahamu kuwa wakristo wengi watakuja kuisahau. Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya Bwana, na tazama, mlangoni pa hekalu la Bwana, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la Bwana, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki                                                              (Ezekieli 8:16)
( Jumapili ni Sun + Day = Sunday, siku ya jua).

Ni amri ndefu kuliko zingine zote 10
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa
.
                                                                                          ( Kutok 20:8-11)

Mungu amerudia mara mbili kirai “ …fanya kazi kwa siku sita” na “…siku ya Saba ni Sabato ya Bwana…” Hii ilikuwa ni kuonesha “UMUHIMU WA SIKU HII”
Je, Yesu aliitunza Sabato ???
Ndiyo, Yesu aliitunza Sabato
       Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.
(Marko 1:21) “Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?” (Marko 6:2)

        Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. ( Luka 4:16) Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato(Luka 4:31). Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. ( Luka 13:10) Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza.           ( Luka 6:6)

Je, ni kweli kuwa Sabato iliishia msalabani ???

Sabato ya amri ya nne haikuishia msalabani. Ni agano la milele Kut. 31 :16. Sabato iliyoishia msalabani, ilitokana na amri za Musa, amri ambazo ziliwaongoza Waisrael kutii Amri 10 za Mungu. Angalia tofauti zake ;

Tofauti ya Amri za Mungu na za Musa
Amri za Mungu Amri za Musa
1. Ziliandikwa na Mungu mwenyewe.
Ziliandikwa na Mungu mwenyewe kwa  kidole chake Torati 31:18 kwa kidole chake, Kutok 31:18
2. Ziliandikwa kwenye mbao mbili .Ziliandikwa kwenye mawe yaliyochongwa, Torati 10:1-4 chuo (kitabu cha dini),Torati 31:24
3. Ziliwekwa ndani ya Sanduku la Agano Torati 10:1-4 ziliwekwa nje pembeni ya Sanduku la Agano,Torati 31:24-27
4. Waliozivunja, walionekana kutenda dhambi. Waliozivunja, hawakuonekana na dhambi 1Yoh. 3:4, na iliwapasa dhambi wala haikuwapasa kufakufa. Torati 17:2-5 kwani zilikuwa ni kivuli cha Kristo.Wakolosai 2:14-17
5. Yesu alikuja kuzitimiliza wala si ku zitangua . Watu wote wanapaswa kuzifundisha maana zilikuwa ni sheria za maagizo tu yaliyosimama kama kivuli cha mema yajayo. Mathayo 5:17-19 Kolosai 2:15
6. Sheria(torati) ya Bwana ni takatifu. Zilikuwa ni kivuli cha kazi njema na ya haki, nayo yadumu mi lele na milele, Yesu aliyoifanya msalabani.  Warumi 7:12 zilikomea hapo. Ebran. 10:1-12
7. Sheria za Bwana ni kamilifu, za 7. Ziliishia pale Kristo alipokufa adili, kweli na za milele. Msalabani. Waebran. 9:10-12, Zaburi 111:7-8 Luka 22:37

A. Mfano wa sheria ya Musa
Kuchinja kondoo kama mbadala wa mdhambi. Kutoka 29…, Walawi, Torati, Nyakati nk
Kifo yeyote aliyevunja mojawapo au Amri zote 10 za Mungu. Kutoka 31:14… Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.
B. Sheria za Mungu, Kutoka 20 :1-17
Hivyo basi Yesu alipokufa Msalabani sheria za kuchinja kondoo tena ziliisha maana mwanakondoo wa Mungu (Yesu) aichukuaye dhambi ya ulimwengu alikuwa ameshachinjwa tayari.
Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Yohana 1:29.

Kama kifo cha Yesu msalabani kilibadilisha Sabato, tuangalie Mitume wake waliabudu siku gani ??
Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi.
                                          ( Mdo 13:14)

Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu. (Mdo 13:27)
Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili. (Mdo 13:42)
Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. (Mdo13:44)
Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi. (Mdo 15:21)
Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. (Mdo 16:13)
Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu. (Mdo 17:2)
Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani. (Mdo 18:4)

1. Paulo bado anasisitiza Waebrania 4:9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.
2. Isaya anasema hadi mbinguni, tutaitunza Sabato ya Bwana
“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana”. ( Isaya 66 :22, 23)

Kwani siku ya Sabato in Ipi ??
“Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.”
(Mathayo 28:1)
“Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza” (Marko 16:2). “Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.” (Marko 16:9).Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. (Luka 24:1)
“Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.” ( Yohana 20:1)
       “Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu” (Yohana 20:19)


Yesu alifufuka siku ya jumapili ambayo Biblia inaiita kuwa ni siku ya kwanza ya juma. Kama Yesu alifufufuka siku ya kwanza ya juma(jumapili), Sabato itakuwa lini??
Jibu: Jumamosi
Upendo wetu kwa Yesu
Je, mtu anaweza kumpenda Yesu bila kushika Amri zake 10???
Hasha!! Yeye anasema; mkinipenda mtazishika amri zangu
   (Yoh 14:15)
(Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake).  (Yohana 14:21)
(Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake). (Yohana 15:10)

Je, inawezekana kushika Amri 9 tu isipokuwa Sabato???
Hasha!! Haiwezekani kabisa, Biblia inasema;
Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. (Yakobo 2:10)
Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake. (1 Yohna 2:3-5)

Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. (1 Yohana 5:2-3)

Wateule wa Mungu ni wapi???
Ni wale wamwaminio na wampendao Yesu kwa kuzishika Amri zake. Hapo ndipo penye subira ya watakatifu wale wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu.  (Ufunuo 14:12.)

Karibu tujiunge kwenye kundi dogooo. Kundi dogo liendalo Uzimani.
      Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. (Mat 7:13-14)
Mwenye sikio, na asikie.
Nawaombea Mungu awafungue akili zenu.

No comments:

Post a Comment