WAKRISTO NA SIKU ZAO ZA IBADA UTANGULIZI


Sababu za wakristo na siku zao za kuabudu.

Nilipata kuyasoma mafundisho yaliyoandikwa na wachunngaji hawa wanaoonekana hapo juu, ambayo yalinifanya kwa namna moja au nyingine nifanye uchambuzi juu ya mambo haya mazito. Ningepena pia kukushirikisha japo kwa uchache ufafanuzi na mafundisho mbalimbali yanayohusiana na mada hii, yakiwemo pia mawazo ya watu mbalimbali nilioweza kuyaona kwenye mitandao ya kijamii. 


Karibu na jumuika nami tujifunze pamoja juu ya mambo yanayotutatiza. Naanza kwa kunukuu sehemu ya chapisho lake juu ya mada hii ya Sababu za wakristo kuabudu Jumapili ambayo ulimwengu umebaki hawana jibu la uhakika.

Mchungaji aliandika hivi:-

"Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka [UFUNUO1:10] Tunaitenga maalum kumwabudu Bwana kwa sababu:-
  1. Ni sikukuu ya malimbuko ya mavuno ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, SIKU YA PILI baada ya Sabato; Ikiwa ni utabiri wa Kristo ambao ni LIMBUKO lao waliolala                                                                             [WALAWI23:9-14;1WAKORINTHO15:20].
  2. Ni siku ya ushindi ya Bwana wetu Yesu aliyofufuka, na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwa Yesu                        [YOHANA 20:1,19,26 WARUMI 10:9].
  3. Siku ya kuja Roho Mtakatifu, Mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika kanisa, ilikuwa siku ya Pentekoste ambayo ni Jumapili, siku ya pili baada ya Sabato                                                                   [MATENDO 2:1]
  4. Siku ya Pentekoste, Jumapili ndiyo siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza lilianza mahubiri na watu 3,000 wakaokoka na kuanza kusanyiko la kwanza la Ibada kanisani                                                                  [MATENDO 2].
  5. Wakristo wa kanisa la kwanza walikusanyika Jumapili                         [MATENDO 20:6-12;1WAKORINTHO 16:1-2].
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.
Hakuna andiko lolote linalosema mtu yeyote anayeabudu Jumapili ana alama ya 666 ya mnyama. Huo ni uzushi. Biblia inatupa uhuru wote katika kuchagua siku ya kumwadhimisha Bwana [WARUMI14:5-6]. Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa siku zote ni siku za kujifunza Neno [MATENDO 17:11;2:46].
KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA
Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:9-10,13]."

Biblia inasemaje? 
Baada ya kusoma kipengele hicho ambacho kinajieleza wazi kuwa Sabato ni lini na kwanini imebadilika kuwa siku ya jumapili badala ya jumamosi? Shauku yangu kubwa ilikua ni kutaka kujua ya kua ni nani hasa aliyepewa mamlaka haya ya kubadili majira na nyakati alizozifanya Mungu? Au pengine labda Mungu mwenyewe ndiye alyeyafanya mabadiliko haya. Sasa tuangalie maandiko mbalimbali na ukweli juu ya swala hili, 

 MAELEZO HAYA YAMETOKANA NA TAFITI MBALIMBALI NA NUKUU MBALIMBALI KUTOKA KWENYE VITABU MBALIMBALI VYA HISTORIA YA DUNIA VINAVYOELEZA JUU YA HISTORIA YA KUGAWANYIKA KWA DINI NA MADHEHEBU YAKE.

Tafadhali soma kwa makini juu ya ukweli wa swala hili kwenye blog hii.


 Posted by Fortune A.

No comments:

Post a Comment