Moja ya dhana kuu katika Agano Jipya ni kwamba
Yesu Kristo alikuja kufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu na kutoa ukombozi kwa
ulimwengu uliokatwa kutoka kwa Mungu.
Mkuu wa kughushi (mwovu Shetani, aitwaye
“mungu wa ulimwengu huu” katika 2 Kor. 4:4) hutafuta kughushi kila
kipengele cha mpango wa Mungu. “Audanganyaye ulimwengu wote” (Ufu. 12:9). Akiwa
mdanganyifu mkuu, asingeridhika kughushi vipengele vingine vya Ukristo
na kuacha utambulisho na ibada ya Mwokozi wa kweli!
- “Mwokozi” halisi katikati ya desturi ya “Isita” ni nani?
- Je, ni yule Yesu Kristo wa Biblia?
- Kama unasema “ndiyo,” una uhakika?
Kisha hii: “Mara nyingi imedaiwa kwamba imani
hii katika Kufufuka kwa Yesu ni kwa sababu ya fikira za ufufuo wa kiungu
zilizoko ulimwenguni sasa…simulizi za Attisi, Adonisi, na Osirisi…Katika
simulizi za kipagani kufufuka tena ni upinduaji wenye furaha dhidi ya
kushindwa, katika simulizi ya Kikristo ni kamilisho la kifo cha ushindi.
Inaweza kusemwa kwamba Attisi na Osirisi waliokoa kwa kufufuka tena, Yesu kwa
kufa…ushikaji wa Isita haukutokea mara moja kutokana na imani katika Ufufuo,
bali ulianza baadaye kwa hatua za taratibu kutoka kwenye Pasaka ya Kiyahudi.
Dhana inayomaanishwa katika salamu ya Isita Kristo amefufuka ni hatua ya pili ya maendeleo; fikira hii inatoka katika sikukuu hii sambamba na kutokea kwake katika majira ya machipuko; sikukuu haitokani na fikira. Fikira ya kufufuka kwake Kristo ilichomekwa katika kawaida za zamani za ushikaji wa Isita na si vinginevyo” (A. Nock, Ukristo wa Mwanzo wa Watu wa Mataifa na Msingi Wake wa Kihelenisti, ku. 105-107).
Na, hatimaye, dhana nzito ya bandia ambayo hurudiwa mara kwa mara imewekwa wazi zaidi na mwanahistoria maarufu, James George Frazer: “Sasa kifo na kufufuka kwa Attisi vilisherehekewa rasmi huko Roma tarehe 24 na 25 ya mwezi Machi, tarehe ya mwisho ikijulikana kama ikwinoksi [siku mlingano (ambapo jua huvuka mstari wa ikweta na usiku na mchana kuwa sawa)] ya majira ya machipuko, na…kulingana na desturi ya zamani iliyoenea sana kwamba Kristo aliteseka siku ya tarehe 25 ya mwezi Machi…desturi iliyoweka kifo cha Kristo siku ya tarehe 25 mwezi Machi…ni ya kushangaza zaidi kwa sababu maangalizo ya kinajimu huthibitisha kwamba isingeweza kuwa na msingi wa kihistoria…Tunapokumbuka kwamba sikukuu ya Mt. George katika mwezi Aprili imechukua mahali pa sikukuu ya kipagani ya kale ya Parilia; kwamba sikukuu ya Mt. Yohana Mbatizaji katika mwezi Juni imefuatia sikukuu ya kipagani ya maji iliyo katikati ya majira ya Mavuno; kwamba sikukuu ya Kupalizwa Bikra mwezi Agosti imeiondoa sikukuu ya Diana; kwamba sikukuu ya Watakatifu Wote [kufuatia mkesha wa sikukuu ya watakatifu wote (31 Oktoba)] katika mwezi Novemba ni mwendelezo wa sikukuu ya kale ya kipagani kwa ajili ya wafu; na Kuzaliwa kwa Kristo mwenyewe kuliwekwa kwenye mwanzo wa majira ya baridi mwezi wa Desemba kwa sababu siku hiyo ilidhaniwa ni Kuzaliwa kwa Jua; hatuwezi kufikiriwa kuwa na pupa au wasio makini katika kudhani kwamba sikukuu nyingine maalumu ya kanisa la Kikristo—uhalalishaji wa Isita—ulikuwa katika namna ile ile, na kutoka katika nia ile ile ya kurekebisha, kulikofanywa kwenye sherehe inayofanana na ya Attisi mungu wa Kifirijia siku ya 21 mwezi Machi wakati wa majira ya kumea…ni upatanifu wa kushangaza…kwamba sikukuu za Wakristo na watu wa Mataifa za kifo na ufufuo wa ki-mungu vyote vingeadhimishwa majira yale yale…ni vigumu kuufikiria upatanifu huu kama kitu ambacho hakikukusudiwa” (Tawi la Kidhahabu, Kit. 1, ku. 306-309).
Tunaweza kufanya muhtasari wa chanzo hicho hapo juu. Kanisa la Kikatholiki la Kirumi lilikuwa na kawaida ya kuingiza sikukuu za kipagani—kwa kuzipachika majina ya “Kikristo” na kuziita za “Kikristo.” Hii ilifanyika ili Ukristo ukubalike na ueleweke zaidi kwa wenye kuabudu miongoni mwa watu wa Mataifa, ambao Kanisa lilikuwa likijaribu kuwavutia. Ni kwa jinsi gani hali hiyo ya mambo ilianza?

Sasa inaweza kueleweka vizuri zaidi kwa nini
mtume Paulo aliwaandikia Wakorintho wawe macho dhidi ya udanganyifu wa kijanja
wa “Yesu mwingine ambaye hatukumhubiri.” Alisema, “Lakini nachelea; kama
yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu,
mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Maana yeye ajaye akihubiri Yesu
mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine
msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali…” (2 Kor. 11:3-4).
Wakati mwingine watu wanaweza kufikiri kwamba wanamwabudu Mwokozi wa kweli wakati kwa hakika wanaabudu mwokozi bandia—Yesu mwingine! Kwa hakika Ukristo wote wa kawaida unamwabudu Baali, mpatanishi na mungu jua, aliyeitwa jina kufuatia “mke” wake Ishita (ambaye kwa hakika alikuwa mama yake Semiramisi)—tutakuja kuona baadaye kuwa ndiye yule Biblia humwita “Malkia wa Mbinguni.”

Watu wanaweza kuabudu katika njia zinazowakilisha
vitu ambavyo ni tofauti kabisa na kile wanachokiamini kwa dhati au kukusudia.
Tafakari mfano huu halisi.
No comments:
Post a Comment