KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA UJANA SEHEMU YA 1

AMNA YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA UJANA

September 7, 2014
1
Shalom, neno changamoto linaweza kuwa na maana kadhaa, katika somo hili nimefafanua changamoto kama ushindani au mashindano baina ya pande mbili au zaidi, kila upande ukidai uhalali wa kile unachokiamini na hivyo kushawishi upande wa pili ukubaliane na kukifuata kile unachokiamini. Kutoka kwenye dhana ya vita vya kiroho (Waefeso 6:10), Shetani kama mfalme wa giza ndiye mwenye kuzileta changamoto mbalimbali dhidi ya wana wa Mungu kwa nia ya kuwaondoa kwenye nafasi zao za ki-Mungu na hivyo kuwatumia kufanikisha makusudi yake ya ufalme wa giza na mwishowe kuwaharibu kabisa. Zifuatazo ni sehemu ya changamoto kubwa zenye kuwakabili vijana;
  •  Kuipenda dunia (1Yohana 2:15 -16).
Ule mstari wa 15 unasema ‘Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia, Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake’. Sisi sote leo tu mashahidi juu ya nama ambavyo vijana wengi, wanavyovutwa na nguvu ya dhambi inayotenda kazi duniani kupitia taama ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima. Shetani kwa kutumia mambo hayo amewafanya wengi sana kuipenda na kuifuatisha namna ya dunia hii, wasijue kwamba nia ya mwili ni mauti na wale waufutao mwili hawawezi kumpendeza Mungu (Warumi 8:5-6)
  •  Kufanya maamuzi muhimu yahusuyo maisha
4
Vijana wengi wapo katika rika ambalo wanahaja ya kuoa au kuolewa na wengine bado wanasoma katika nagzi mbalimbali. Katika nyakati za sasa imeakuwa ni changamoto kubwa sana kwa kijana kumpata mwenza shaihi wa maisha sambamba na kujua nini asome ambacho kina uhusiano mkubwa na wito wa kusudi la Mungu katika maisha yake. Tambau kwamba (a) Mungu anapokupa fursa ya kusoma, si suala la kusoma bali kusoma kitu ambacho kipo connected na future ambayo Mungu amakuandalia (b) si kila mwanamume/mwanamke anafaa kuwa mwenza wako wa maisha. Naam ile kwamba wako wengi ambao wangetamani kuishi na wewe kama mke au mume ni ishara kwamba wengi wao si wenza sahihi wa kuishi na wewe. Katika kutafuta na kupata mwenza wa maisha vijana wengi leo wanatumia akili zao bila kumshirikisha Mungu ipasavyo, wasijue kwamba ndoa isiyounganishwa na Mungu, ni kikwazo kikubwa katika kulitumikia shauri la BWANA Mungu wao.
  • Kuishi kwa amani katika ndoa 
Wanandoa
Hii inahusu wale ambao walishaoana. Kwa zaidi ya miaka saba katika kufundisha na kuandika masuala yahusuyo mahusiano ya wanandoa nimejifunza na kuthibitisha kwamba ndoa nyingi za vijana zina matatizo makubwa kuliko wengi wanavyofikiri juu ya ndoa hizo ambazo wanaamini ni changa. Binafsi nimeshuhudia ndoa nyingi ambazo ni chini ya miaka mitano lakini wanandoa husika hawalali kitanda kimoja tena, hawaaminiani tena, hawapeani unyumba tena nk. Naam kuishi vema na mwenza limekuwa gumu sana kwa wanandoa wengi ambao ni vijana na baadhi yao wanajuta kwa nini walioa au kuolewa.
  • Matumizi ya teknolojia (mtandao)

2Kijana mwenzetu Danieli alionyeshwa kwamba katika siku za mwisho maarifa yataongezeka sana, jambo ambalo ni dhahiri katika kizazi chetu bila shaka. Sote tu mashahidi juu ya namna vijana wanavyotumikishwa na nguvu ya matumizi mabaya ya mitandao mbalimbali ya kijamii. Sote tunaona namna vijana wengi wanavyotumia muda mwingi kusoma na kuangalia vitu visivyofaa kwenye mtandao na mbaya zaidi tunaona ni kawaida. Kadri kijana anavyaongalia vitu vichafu ndivyo anavyoyachochea nguvu ya dhambi na kutenda mabaya ndani yake, naam ndivyo anavyoingiza roho chafu za kila namna ndani yake.
  • Kijana na maisha/uchumi
Hali ngumu ya kiuchumi inaleta ushawishi kwa vijana kujiingiza kwenye mambo ambayo yanaharibu mahusiano yake na Mungu. Naam wapo ambao imefika mahala wameamua kuingia kwenye biashara haramu za madawa ya kulevya, zinaa, uasherati, kutamani kuishi maisha ya kuiga, na mbaya zaidi hata wale ambao wanakiri kumpokea Yesu nao wanaishi maisha ambayo hayana ushuhuda makazini mwao, mtaani mwao nk hususani linapokuja suala zima la uaminifu, mahusiano na fedha.
Pengine zipo changamoto nyingine, lakini hizi tano nilizoziandika ndizo ambazo nimeona umuhimu wake zaidi kuzifundisha kwa kuwa zina athari kubwa sana sit u kwa vijana wenyewe bali zaidi kwenye ufalme wa Mungu wetu. Katika sehemu ya pili nitaanza kwa kukuonyesha ni kwa namna gani kijana anaweza kuazikabili changamo husika.
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA!

No comments:

Post a Comment