KRISTO NDANI YAKO


Kristo ni yote katika wote. Yeye Menyewe ni yote unayo hitaji—na yote ulimwengu unahitaji pia.Na Yeye yu tayari ndani yako! Kwa hivyo epu tutambue Yesu aishiye ndani yetu!
Ufunuo wa Kristo
Agano jipya lina simamia ufunuo wa Kristo aliye fufuka na kutukuka! Hata wale waliomjua Yeye katika mwili walipaswa kujifunza kumjua katika njia tofauti.Yeye hayupo hapa katika mwili, na Paulo anafanya lengo la jambo kuu kuonyesha yule Aliyefufuka sasa yupo katika mtizamo wetu.
1 WAKORINTHO 15:14—- “tena kama Kriato hakufufuka, bsi kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure”
2 Wakorintho 5:16-17 “ Hata imekuwa,sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye mtu awaye yote kwa jinsi mwili, Ingawa sisi tumemtumbua Kristo kwa jinsi ya mwili,lakini hatumtambui hivi tena.Hata imekuwa,mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya ;ya kale yamepita tazama 1 yamekuwa mapya.”
Zoezi la Kristo lote sasa limeingia hatua ingine ; Yohana 14:19 “Bado kitambo kidogo na ulimwengu hauninoni tena, bali ninyi mnaniona.Kwa sababu mimi ni hai ninyi nanyi mtakuwa hai.”
Haya ni mahubiri ambayo kiini chake ni Yesu, ambako kila kipo ndani ya Kristo.
Kila hazina ya maarifa na hekima ipo na imefichwa katika Yeye.Katika Yeye ukamilifu wa Mungu kama kichwa waishi ndani yake katika umbo la mwili. Kristo ni yote, na katika yote.
Wakolosayo 2:2-3,2:9-10,3:3-4 na 3:11
Christ Kristo – ni nguvu za Mungu na Hekima ya Mungu
Tuna mhubiri Kristo; Yeye ni nguvu za Mungu na hekima ya Mungu,katika Yeye ahadi zote za ni ndiyo, na Krsito ni uzima wetu. Tupo ndani Yake na Yeye ndani yetu (2 wakorintho 1:19-20 na Yohana 15:4-5 )
1 Wakorintho 1:30-31 bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, alye fanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aoneye fahari na aone fahari juu ya Bwana.”
Ufunuo wa “Kristo kuwa siri ya Mungu” ni sehemu kuu ya ujumbe ulifunuliwa kwake Paul. (Wakolosayo 2:2-3 ) maneno ya muhimu “ katika Yeye” yananukuliwa katika nyaraka za Paulo mara mia moja zaidi! Hii ni kwa sababu siri ya injili imefichwa katika kweli hii.
Na katika nuku yale A B Simpson “ Yeye mwenyewe” ni ajabu.Alipo mtambua Kristo, kila kitu kiweza kubadlika na kubatilizwa! Soma hii habari inayo julikana imebariki mamilioni ya Wakristo duniani kote: www. GlobalGraceNetwork.com /absimpson
Ufunuo wa Kristo ndani yetu
Kweli kuhusu “ Krsito ndani yetu” ni kiini cha kweli ya injili. Wakati Paulo alipewa uwakili wa kutimiliza neno la Mungu, na kufunua siri iliyokuwa imefichwa tokea vizazi na vazazi, ilikuwa juu ya haya, ... “Siri iliyo fichwa tangu zamani zote ba tangu vizazi vyote,bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katiaka Mtaifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu. ambaye sisi tunahubiri habari zake tukimwonya kila mtu,na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.” Wakolosoya 1:26-28
Tunapo tambua ya kwamba Kristo ndani yetu ndiye ufunguo, hapo tunatambua “ mimi ni mpya, ” Maana mimi nimesulubishwa na na Kristo, na siishi mimi tena na maisha ninayoishi, ni maisha “Kristo akiwa ndani yetu,”
Wengine wanashida katika kupokea huu ujumbe.Wanafikiri, na je itakuwaje kuhusu talanta na karama, hazina yangu na kile Mungu ameweka ndani yungu? Je hii haitaweza kutambulikana?
Kristo ni maisha yetu. Tupo ndani yake na Yeye yupo ndani yetu.
Hapa kuna jawabu, Wewe unakuwa sehemu ya mwili ; unakuwa mshirika na Kristo. Hii haimhusu mtu wowote, ila ni kuhusu Yeye.Kwa hivyo amekupa kitu kitakacho fikia ukamilifu wake, utakapo zama ndani Yake.
Mimi aliye mpya, ni “ Kristo ndani yako;” kwa uhakika iko ndani yake uweza wako wote, karama, chombo na uumbaji.Lakini utukufu wote na heshima ni wa Yule afanyaye kazi ndani yetu. Wakati theluji inapo anguka kila moja inakuwa mzuri, inang’aa na ya ajabu.Hakuna inayo fanana!, Walakini, sivyo inapo unguka ndipo inatimiliza huduma wake kikamilifu. Licha ya kuwa za kupendeza. Ni wakati tu barafu inapokuwa pale imezambaa kama mkeka juu ya nchi ndipo kila sehemu ya hiyo theluji ipo katika chembe yake sawasawa.
“Kufichwa na Kristo katika Mungu” ni mahala pa utukufu!



Utukufu wa mungu hung’aa toka ndani mwetu
Tunapo kuwa na Kristo ndani mwetu, Nuru hung’aa moyoni mwetu, Yeye mwenyewe ndiye nuru! Alafa utukufu wa Mungu uliyopo ndani ya uso wa Yesu Kristo, hung’aa toka kwetu. Hii ni njia ya Mungu kuangazia nia ya wasio amini, maana Mungu wa Kizazi hiki amepufusha macho yao.
Tuna hasina hii katika vyombo vya udongo, ili ubora wa uweza wake uwe wa Mungu, na sio wetu sisi. Lakini Kristo ndani yetu, maisha ya Yesu pia yanaweza kufunuliwa kupitia mwili wa kawaida!
Huu ndiyo ufunuo! Yeye anaishi ndani yetu, anatembea ndani yetu, Kristo, yeye anaye jua jinsi ya kuishi maisha Kikristo!
Katika nyakati zilizo pita, alikuwa Immanueli, Mungu pamoja nasi.Alikuwa na sisi na akaishi miongoni mwetu. Walakini, wakati agano jipya lilikuja, akaja ndani mwetu, Yohana 14:20 siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu ; nanyi ndani yangu yenu.
Yohana 15:4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi livivyoweza kuzaa pekee ndani ya mzabibu ; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
Bila Yeye hatuwezi kafanya chochote, lakini ndani Yake tunaweza kufanya vyote. Uwepo wake ndani yetu mwetu ndiyo utakatifu uliyopo. Hii ndio siri ya injili.
Ushuhuda wa “ Kristo ndani Yetu“
Ray McCauley anachunga kanisa kubwa kule Afrika Kusini.Siku moja alipo amrisha pepo chafu kutoka ndani ya mtu yule pepo,alisema “ Mimi siwezi kuondoka ila kwa maombi na kufunga ; na wewe hauja funga kwa hivyo siondoki,” Hii ndiyo mbinu ya ukweli wa ibilisi, akijaribu kuipa imani yetu kwa kufanya mtizamo wetu kutulenga sisi wenyewe.
Licha ya haya Yesu alimpa huyu mchungaji hekima na akajibu; “ndiyo, nimefunga, maana Yesu ndani yangu ameshafunga siku 40 na usiku 40, na katika jina lake lazima utoke! Na bila shaka yule pepo akamtoka.
Kwa hivyo tusijiangalie sisi wenyewe na kuona iwapo ni haki yetu, jitihada letu, upendo au imani ni mzuri zaidi.
Uzima wetu umefichwa ndani ya Kristo, na sio unao hesabika tena. Kristo sasa amekuwa uzima wetu! Wakolosai 3;3-4, Wagalatia 2:20.Hii inamaanisha ya kwamba, sio imani yetu inayo hesabika tena, lakini ni imani ya Yesu ndani yetu. Sio haki yetu sisi wenyewe inayohesabiwa tena, lakini Yeye mwenyewe ndiyo sasa haki yetu, amani, furaha, upendo,tumaini,imani,uweza, nuru na uzima. Yeye ni mponyaji pia Yeye mwenyewe ni uponyaji. Yeye ni yote tunayo weza kuhitaji.

No comments:

Post a Comment