MABADILIKO YA SIKU ZA IBADA SURA YA 5

SURA YA 5
JUMAPILI NA IBADA YA JUA
Amri iliyowekwa na Konstantino ya kuanzisha uadhimishaji wa Jumapili inatajwa na vitabu viwili vya insaiklapidia (encyclopedias):

"Utambuzi wa kwanza kuliko wote wa uadhimishaji wa Jumapili kama wajibu wa kisheria ni
amri ile ya Konstantino ya mwaka 321 B.K., iliyoamuru kwamba mabaraza [mahakama] yote ya sheria, wakazi wote wa mijini, na viwandani wanalazimika kupumzika siku ya Jumapili (VENERABILI DIE SOLIS [SIKU TUKUFU YA JUA]), isipokuwa  upendeleo maalum ulitolewa kwa wale waliokuwa wanashughulika na kazi ya kilimo."
                                                 ENCYCLOPAEDIA BRITANNICA (llth ed.), art. "SUNDAY."
Kwamba amri hii ya Jumapili haikuwa na uhusiano wo wote na Ukristo ni dhahiri kama mambo yaliyomo katika kifungu cha maneno kifuatacho kilichonukuliwa yatazingatiwa:

"Amri hii iliyotolewa na Konstantino pengine haikuwa na uhusiano wo wote na Ukristo; kinyume chake, inaonekana kwamba Mfalme huyo katika uwezo wake kama Kuhani Mkuu (Pontifex Maximus), alikuwa anaongeza tu siku nyingine ya jua, ambayo ibada yake ilikuwa imeimarishwa sana katika Dola yote ya Warumi, juu ya siku zile nyingine za kishenzi [kipagani] za kalenda yao takatifu." 
                                               HUTTON WEBSTER, Ph.D., REST DAYS, uk.122, 123.
KUIMARISHA UTUNZAJI WA JUMAPILI KWA AMRI
Kufuatia amri hiyo ya awali, wafalme wote na mapapa wote katika karne zile zilizofuata
waliongeza amri nyingine za kuimarisha utunzaji wa Jumapili.

"Walakini, kile kilichoanza kama amri ya  kipagani, kikaisha kama amri ya Kikristo;
msururu mrefu wa amri za kifalme katika karne ile ya nne, ya tano, na ya sita, zikaamuru kwa
ukali kujizuia kufanya kazi siku ya Jumapili." 
                                                                Kitabu kile kile (ibid.) uk.270.
Hatua hizi za ziada ambazo kanisa na serikali walizichukua kuhakikisha ya kwamba Jumapili inakuwa badala ya Sabato kwa lazima, zimeelezwa katika aya chache tu na mwanasheria maarufu wa Baltimore, Maryland, aitwaye James T. Ringgold:

"Katika mwaka 386, chini ya Gratian, Valentinian, na Theodosio (Theodosius), iliamriwa
kwamba mashauri [daawa] yote mbele ya sheria pamoja na shughuli zote hazina budi kukoma
[siku ya Jumapili]....

"Miongoni mwa mafundisho ya dini  yaliyoandikwa katika waraka wa Papa Innocent I, ulioandikwa katika mwaka wake wa mwisho wa upapa (4l6), ni kwamba siku ya Jumamosi [Sabato] iadhimishwe kama siku ya kufunga [kuacha kula chakula] tu....

"Katika mwaka 425, chini ya Theodosio Kijana, kujizuia kufanya michezo ya kuigiza (theatricals) pamoja na kutofanya tamasha (circus) [Jumapili] kuliamriwa....

"Mwaka 538, katika Baraza la Orleans,... iliagizwa kwamba kila kitu kilichoruhusiwa siku za nyuma kufanyika siku ya Jumapili kiendelee kuwa halali; bali kwamba kazi ya kulima kwa plau, au katika mashamba ya mizabibu, kukata majani, kuvuna, kupura nafaka, kulima, na kuweka boma la miti viepukwe kabisa, ili watu waweze kuhudhuria kanisani kwa raha zaidi....

"Karibu na mwaka 590 Papa Gregory, katika waraka wake kwa Warumi, aliwashutumu kuwa ni manabii wa Mpinga Kristo wale waliosisitiza kuwa kazi isingepaswa kufanywa siku ile ya saba." 
THE LAW OF SUNDAY, Uk..265-267.
Aya ya  mwisho ya kufungia maneno yaliyonukuliwa juu huonyesha kwamba bado walikuwamo ndani ya kanisa hadi kufikia mwaka 590 B.K. wale ambao walikuwa wanaitunza na kuwafundisha wengine kuitunza Sabato ya Biblia. Kusema kweli, utunzaji kama huo kwa wale wachache umefuatwa katika karne zote za Kikristo. Miongoni mwa wale walioitwa Waldensia (Waldenses) walikuwamo watunzaji wa siku ya saba.

Neander anauliza swali hili:
"Je, tusiweze kudhani kwamba tangu zamani za kale kikundi cha Wakristo wanaofuata desturi za Kiyahudi kilisalia, ambacho kutokana nacho madhehebu hii [ya Wapasaginia (Pasaginians), waliowekwa katika kundi moja na Waldensia na baadhi ya waandishi wanaoaminika] inapaswa kufikiriwa kama tawi lao?"   CHURCH HISTORY, FIFTHPERIOD, Section 4, 15th American ed., Vol. IV, uk. 591.
Amri za kidini na serikali zilizotajwa sasa hivi katika kuianzisha amri ya Jumapili zinaliweka suala hili kwa wazi sana hata Eusebio, Askofu maarufu wa Kanisa Katoliki, baba mmoja mwenye kusifika wa historia ya kanisa, na mwenye mazoea ya kujipendekeza mno kwa Konstantino na mwandishi wa habari za maisha yake, alikuwa na haki kusema hivi:

"Mambo yo yote ambayo yalikuwa ni wajibu kufanyika siku ya Sabato, hayo sisi tumeyahamishia katika Siku ya Bwana [Jumapili]."
COMMENTARY ON THE PSALMS, COMMENT ON PSALMS  9l (92 IN AUTHORIZED VERSION), quoted in ROBERT COX, LITERATURE OF THE SABBATH QUESTION, Vol.I, uk. 36l.

KUIWEKA SIKU YA KIPAGANI MAHALI PA SIKU YA MUNGU
Huku kuiweka Jumapili  badala ya Sabato sio jambo ambalo Kanisa Katoliki linakana au linajaribu kuficha. Kinyume chake, linakiri wazi, na kwa kweli linaonyesha kitendo hicho kwa majivuno kuwa ni ushahidi wa uwezo wake wa kubadili hata amri ya Mungu.

Soma maneno haya yaliyonukuliwa kutoka katika Katekesimo za Kikatoliki:

THE CONVERT'S CATECHISM OF CATHOLIC DOTRINE, kazi ya Reverend Peter
Geiermann, C.S.R., Januari 25, l9l0 ilipokea "mbaraka wa kitume" wa Papa Pius wa X. Juu ya somo hili la badiliko la Sabato, Katekesimo hii inasema hivi:
"SWALI. ----- Siku ya Sabato ni siku gani?
"JIBU. - ---- Jumamosi ndiyo siku ya Sabato.
SWALI.
Kwa nini tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi?
JIBU.
“Tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu Kanisa Katoliki, katika Baraza la Laodikia (336 B.K.), lilihamisha taratibu ya ibada kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.”           (Toleo la pili, uk. 50.)

A DOCTRINAL CATECHISM, iliyoandikwa na Reverend Stephen Keenan, iliidhinishwa
na Most Reverend John Hughes, D.D., Askofu Mkuu wa New York. Inayo maneno haya
kuhusu suala hili la badiliko la Sabato:
SWALI.
Unayo njia nyingine yo yote ya kuthibitisha kwamba kanisa linao uwezo wa kuanzisha sikukuu ambazo zinashikwa kama amri?
JIBU.
“Kama lisingekuwa na nguvu kama hizo, lisingaliweza kufanya kile ambacho wanadini wote wa siku hizi wanakubaliana nacho…………. lisingaliweza kuweka utunzaji wa Jumapili siku  ya kwanza ya juma mahali pa utunzaji wa Jumamosi siku ya saba, badiliko ambalo halina Maandiko yo yote yanayolipa kibali hicho."                                (Ukurasa l74.)
AN ABRIDGMENT OF THE CHRISTIAN DOCTRINE, iliyoandikwa na Reverend Henry
Tuberville, D.D., wa Chuo cha Douay, Ufaransa, ina maswali na majibu haya:
SWALI.
Unathibitishaje wewe kwamba kanisa linao uwezo wa kuamuru sikukuu na siku takatifu?
JIBU.
“ Kwa kitendo kile kile cha kuibadili Sabato kuwa Jumapili, kitendo ambacho Waprotestanti wanakikubali; na kwa hiyo wanajikanusha wenyewe kijinga, kwa kuitunza Jumapili kwa ukali, na kuzivunja karibu sikukuu nyingine nyingi sana zilizoamriwa na Kanisa
lilo hilo.”
SWALI.
 Unalithibitishaje hilo?
JIBU.
“Kwa sababu kwa kuitunza Jumapili, wanaukiri uwezo wa Kanisa wa kuamuru sikukuu, na kuziamuru chini ya sharti  la dhambi; na kwa kule kutozitunza zile zilizobaki [katika sikukuu] ambazo zimeamriwa nalo, kwa kweli, wanaukana tena uwezo ule ule." (Ukurasa 58.)

USHAHIDI WA JUMAMOSI KUWA SIKU YA SABA.
Hebu tuanze na Encyclopedia Britannica Article;
Kinasema hivi:-
“For a time the Romans used a period of eight days in civil practice, but in AD 321 Emperor Constantine established the seven-day week in the Roman calendar and designated Sunday as the first day of the week. Subsequent days bore the names Moon's-day, Mars's-day, Mercury's-day, Jupiter's-day, Venus'-day, and Saturn's-day. Constantine, a convert to Christianity, decreed that Sunday should be a day of rest and worship”
Sunday
Is the first day of the week; in Christianity, the Lord's Day, The emperor Constantine (d. 337), a convert to Christianity, introduced the first civil legislation concerning Sunday in 321, when he decreed that all work should cease on Sunday, instead of Saturday except that farmers could work if necessary.
This law, aimed at providing time for worship, was followed later in the same century and in subsequent centuries by further restrictions on Sunday activities.
Sisi tunasadiki kwamba Biblia inasema kweli. Biblia ndiyo inayoamuru  utunzaji wa sikya saba ya juma.  Siku ile ile ya saba inaweza kupatikana kama mtu ye yote anataka kuitafuta.Nayo inaweza kupatikana hata kama mtu ye yote anataka kuipoteza.  Jua linapotua [linapozama] siku ya Ijumaa jioni, siku ya saba ya Uumbaji ile ile inaanza kuingia. Ni siku ile ile ya saba ambayo amri ya Mungu inatuagiza kuitunza. Amri ile inatangaza kwamba, "Siku ya  saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote." Kwa hiyo, jua litakapotua Ijumaa hii ijayo wakati wa jioni, utakuwa umeingia katika saa takatifu.

Asante, na Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment