UBATIZO
Utangulizi
"Mtu YEYOTE
akiyaongeza Mungu Atamwongezea hayomapigo yaliyoandikwa KATIKA kitabu HIKI Na
MTU YEYOTE akiondoa lolote ktk Maneno ya UNABII wa kitabu HIKI Mungu
atamwondolea sehemu KATIKA ULE mti wa uzima Na KATIKA ULE miji mtakatifu AMBAO
habari zake zimeandikwa KATIKA kitabu hiki" Ufunuo 22:18b-1.
UBATIZO NI NINI??✍
"hamfahamu ya
kuwa sisi sote tuliobatizwa KATIKA kristo Yesu tulibatizwa KATIKA mauti yake?.
BASI TULIZIKWA PAMOJA NAYE KWA NJIA YA UBATIZO KATIKA MAUTI YAKE KUSUDI KAMA
KRISTO ALIVYOFUFUKA KATIKA WAFU KWA NJIA YA UTUKUFU WA BABA VIVYO HIVYO NA
SISI TUENENDE KATIKA UPYA WA UZIMA. Warumi6:3-4
“Basi tulizikwa
pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama kristo
alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi
tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana
kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kuunganika naye;
tukijua nano hili, ya kuwa utu wetu wa kale
ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie
dhambi tena”. Rum 6:4-6.
Kwa hiyo kubatizwa
ni kuzika utu wa kale (Galatia3:27 )maana ninyi nyote mliobatizwa katika kristo
mmemvaa kristo.
Ubatizo huonyesha
mambo muhumu matatu:-
- Kuifia dhambi.
- Kuzaliwa upya katika Kristo.
- Kumpokea Kristo molele.
Ubatizo ni lazima
uendane na imani ya kweli. Maana wote wenye imani ya kweli ni watoto wa Mungu,
1Yoh. 5:4. “Kwa
maana kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huko ndiko kuushinda
ulimwengu, hiyo imani yetu”.
Vivyo hivyo ubatizo
huambatana na imani biblia inasema kuwa mtu ni lazima aamini ndio kasha
abatizwe, mtu hawezi kubatizwa ili hali
hajui wala haamini kwa kile atakachokipokea…. “Aaminiye na kubatizwa ataokoka”
(Mk.16:16)
Hii ni sawa na
kusema kuwa mtoto asijaribu kutembea mpaka awe na uhakika kuwa hatateleza na
kuanguka .
MTU ANAYETAKIWA
KUBATIZWA ANATAKIWA AWE KAMA IFUATAVYO
Aaminiye Na kubatizwa ataokoka asiye amini atahukumiwa..... marko16:15 ✍ NB:Kumbe anayetakiwa kubatizwa sharti aamini he hai
wanaobatiza watoto wadogo wanakuwa wale watoto wamemwamini Yesu kristo awe
bwana Na mwokozi wa Maisha Yao????
Neno la Kigiriki Babtiso ndio msingi wa neno ubatizo kiswahili baptism
kingereza yaani babtiso zamisha zika funika kwa hiyo leo uwezi fanya Retsim
nyunyiza unidanganye ndio ubatizo tuseme kweli tuache upotoshaji
Mambo muhimu kabla
ya kubatizwa:-
- Mtu huanza kwa kulisikia neno la Mungu; kwa maana Imani huja kwa kusikia. (Rum 10:17)
- Ni lazima kujifunza mambo unayopaswa kuyafanya ili kuikuza imani yake. Enendeni mkayafnye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza…… na kuwafundisha kuyashika yote niliyoyaamuru mimi. (Mt.28:19,20).
- Kasha fanya uamuzi sahihi wa kumfuata Kristo.
- Ni lazima kupata toba na msamaha wa dhambi. “Tubuni mkabatizwe kila mtu kwa jina lake Yesu Kristo, mpate aondoleo ya dhambi.” (Mdo.2:38).
Mtu anapotaka
kubatizwa ni lazima atubu ili kupata msamaha wa dhambi zake, na kuyaanza maisha
mapya ya kiroho yenye uwepo wa Mungu, hii ni kwasababu uwepo wa Mungu hutoweka
kabisa palipo na dhambi. “Tubuni
mkabatizwe kila mtu kwa jina lake Yesu Kristo, mpate aondoleo ya dhambi.”
(Mdo.2:38)
Mtu anapotubu dhambi
husamehewa kabisa na Mungu anasahau kabisa maisha ya awali ya mtu. “Tubuni basi
mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.” (Mdo.3:19).
Utangulizi unasema
atayeongeza...mapigo yanamngoja...
MAZINGIRA YA
KUBATIZIA;
(Ubatizo wa Yesu
"mathayo3:13 wakati huko Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka yordani kwa
yohana ili abatizwe akabatizwa mstari 16""
Je nilazima tuende yordan kubatizwa????
(yohana3:22-23) baada ya hayo Yesu Na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya
uyahudi akashinda huko pamoja nao, akabatiza. Yohana Nate alikuwa akabatiza
huko Ainoni karibu Na salimu.
NB:Tunaona Yesu
alibatiwa yordan lakini akaenda kuwabatiza watu huko nchi ya uyahudi Na Yohana
alikuwa akabatiza huko ainoni kwa hiyo si LAZIMA uende ukabatizwe
yordani.
VIGEZO VYA SEHEMU YA
KUBATIZIA
Yohana3:23 Yohana
naye alikuwa akabatiza huko ainoni karibu Na salimu KWA SABABU KULIKUWA NA MAJI
TELE NA WATU WAKAMWENDEA WAKABATIZWA kwa
hiyo sehemu ya kubatizia LAZIMA kuwe Na Maji tele siyo kwenye KIKOMBE AU BAKULIWADOGO,
SABABU YA KWANINI
HATUBATIZI WATOTO WADOGO
Nitawajibu kuhusu
watoto neno linasema watoto wenu hutakaswa na ninyi yaani wazazi,
Basis wakamletea watoto WADOGO ili awaguse .
akawakumbatia akaweka mikono yake juu yao akawabarikia.. (Marko
10:13,16)
Kwa hiyo YESU
mwenyewe hakubatiza watoto aliwabarikia tu kwa hiyo kuhani anawaombea Baraka.
NAOMBA SANA KILA
ASOMAYE HUU UJUMBE AUANDIKE HATA KWENYE DAFTARI LAKE WAWEZA KUMSAIDIA SIKU
NYINGINE.. HAPO NDIYO UJUWE WAPI WANAFUATA MAANDIKO NA WAPI WANABADILISHA
MAANDIKO YALIVYOANDIKWA ASOMAYE NA ATAMBUE:
MAANA KIPOFU
AKIONGOZWA NA KIPOFU MWENZIYE WOTE WATATUMBUKIA SHIMONI kwa watu hawasomi
biblia Na hawataki kuokoka bwana wanasema wanamwamini Yesu halafu wanabaki huko
kwenye DINI watabuluzwa hadi shimoni""
Mungu anatuonya 2Kor
6:14 "Msifungiwe NIRA pamoja Na wasioamini KWA
jinsi isivyo sawasawa..... 17Basis
tokeni kati yao mkatengwe nao ASEMA bwana siyo Mimi. Wewe umeijua kweli
unang'ang'ania tu.
Yohana 8:31-32 Yesu akawaambia wale wayahudi waliomwaminii nanyi
mkikaa KATIKA neno langu mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli. Tena mtaifahamu
kweli nayo kweli itawaweka huru. Hero kulitendea neno kazi kuliko kuwa
msikiaji.
NB:
Yesu alisema atakaye nionea haya Mbele za watu nami
nitamwonea haya Mbele za Baba yangu Na Malaika zake. Napia akaesma wengi
waatawachukieni si ninyi bali kwa ajili ya Jina language kwa sababu
mnaisema kweli..
Je, walioko jangwani
ambapo hakuna mito wala ziwa neno linasemaje?
Yohana 3:3 “Yesu
akamwambia, "Amen nakwambia, mtu asipozaliwa upya hataweza kuuona ufalme
wa Mungu." Moja ya maana ya
ubatizo ni kuzaliwa upya.
Yesu anaposema
kuzaliwa kwa maji na roho....anamaanisha baada ya tendo la kuzika dhambi kwa
njia ya kufa na Kristo (baptiso)..na kufufuka pamoja naye..unapokea kipawa cha
Roho Mtakatifu na unavikwa vazi la haki ya Yesu.
fungu 8 ni
kudhihirisha matendo ya Roho Mtakatifu kwa mtu aliyemuamini Yesu na
kubatizwa..Kazi za Roho hazichunguziki kwa macho isipokuwa katika vitendo.
Watoto hawawezi
kuonesha tendo hata moja la Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui neno lolote baina
ya Wema na Uovu.
Wewe leo kwa
kujitambua huwezi kujisaidia haja kubwa barabarani unajua si adili jema kwa
sababu Roho ananena nawe...lkn mtoto hajui hilo.
Mtu anapobatizwa
mwili wake hugeuka hekalu la Mungu, yaani huitwa kuunganika kuwa mwili mmoja,
“Ndiyo mlivyoitwa katika mwili mmoja”. (Kol.3:15).
Barikiwa!.
No comments:
Post a Comment