WAKRISTO NA SIKU ZAO ZA IBADA SURA YA PILI


SURA YA PILI
Katika sura hii ya pili nitajaribu kutumia mafungu ambayo yanaonesha kuwa SABATO NI YA KUPUMZIKA,KUABUDU NA KUKUSANYIKA.

“Leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu.” Waebrania 4:7
“Maana sisii tulioamini tunaingia katika raha ile kama vile alivyosema, kama vile alivyoapa kwa hasira yangu, hawataingia rahani mwangu……. Waebrania 4:2

A. SABATO KWA AJILI YA KUPUMZIKA:
(i) “Utafanya kazi siku sita, lakini katika siku ya saba utapumzika; Kutoka 34:21
(ii) “Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya Kustarehe kabisa,takatifu kwa BWANA;
B. SABATO NI KWA AJILI YA KUABUDU:
(i)“Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja KUABUDU mbele zangu,asema BWANA.” Isaya 66:23
“Hata siku ya Sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali;Matendo 16:13
C. SABATO NI KWA AJILI YA KUKUSANYIKA:
(i) “mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa,KUSANYIKO takatifu;
(ii)“Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu WOTE WATAKUJA kuabudu mbele zangu,asema BWANA.”   Isaya 66:23
(ii) na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya Sabato ya pili. Matendo 13:42
(iii) Hata Sabato ya pili, watu wengi karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.Mdo 13:44
D. SABATO NI YA MILELE HAIJAISHA:
(i) “Ombeni,ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya Sabato.” Mathayo 24:20 (Hapa hata Yesu anazungumzia nyakati za dhiki ambazo akiwambia watu juu ya mambo ambayo yangewatukia hata baada ya yeye kupaa akawaambia wanafunzi wake waombe Mathayo 24:3”
(ii) Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. (usipojiamini kuwa umeunganishwa na tawi kuwa Mwisraeli soma
Warumi 11:11-25)
(iii) “Baasi, imesalia raha ya Sabato kwa watu wa Mungu” Waebrania 4:9
(iv) “Kama vile mbingu mpya na NCHI MPYA NITAKAZOFANYA, zitakavyokaa mbele zangu,asema BWANA,ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu WOTE WATAKUJA kuabudu mbele zangu,asema BWANA.Isaya 66:22
Luka, tabibu na mwinjilisti katika kanisa lile la kwanza, anatoa taarifa hii.
“Siku ya Sabato tukatoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani kuwa mahali pa kusali. Tuliketi, tukiongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo”(Matendo 16:13).
Kitabu cha Matendo cha Agano Jipya kinataja mara 84 ilipotunzwa. Sabato hiyo na wafuasi wa Kristo, zote hizo zilikuwa zikitunzwa zaidi ya miaka 14 baada ya ufufuo wa Yesu: Sabato 2 pale Antiokia (Matendo 13:14,42,44); 1 pale Filipi (Matendo 16:13), 3 pale Thesalonike (Matendo 17:2,3), Sabato 78 pale Korintho (Matendo 18:4,11).
Yohana, wa mwisho kufa miongoni mwa wale mitume kumi na wawili, aliitunza Sabato. Aliandika hivi:
“Siku ya Bwana nilikuwa katika Roho”(Ufunuo 1:10).
“Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato”(Mathayo 12:8).

Tuwasikilize walioanzisha Kuabudu Jumapili wanasemaje;
Je! Makanisa Ya Kiprotestanti Yanasemaje?
Hati rasmi zinazotoa muhtasari wa itikadi za madhehebu kadhaa ya Kiprotestanti zinakiri kwamba Biblia haitoi kibali cho chote cha kuitunza Jumapili. Martin Luther, mwasisi wa kanisa la Kilutheri, aliandika katika ungamo la Augusiburgi (Augusburg Confession), sharti la imani la 28, aya ya 9, maneno haya: “Wao [Wakatoliki wa Roma] wanadai kwamba Sabato ilibadilishwa na kuwa Jumapili, siku ya Bwana, kinyume na ile sheria ya Amri kumi,.. wala hakuna mfano wanaojivunia sana kama huo wa kuibadili siku ya Sabato. Ni mkuu, wasema wao, uwezo na mamlaka ya Kanisa, kwa kuwa liliiondoa mojawapo ya zile Amri kumi.”
Wanatheolojia wa Kimethodisti Amosi Binney na Danieli Steele walitoa maoni yao haya:
“Ni kweli, hakuna imani dhahiri ya ubatizo wa watoto wachanga….wala hakuna yo yote ya kuitakasa siku ya kwanza ya juma.” Nukuu kutoka Theological Compend (New York: Methodist Book Concern, 1902), Kurasa 180,181.
         Dk. N. Summerbell, mwanahistoria wa wanafunzi wa Kristo (Disciples of Christ) au Kanisa la Kikristo (Christian Church), aliandika, alisema:
“Kanisa la Roma lilikuwa limeasi kabisa…..Liliigeuza Amri ya Nne kwa kuiondoa Sabato ile ya Neno la Mungu, na kuiweka Jumapili kama siku takatifu” nukuu kutoka A True History of the Christian and the Christian Church, kurasa za 417,418.

WAKATOLIKI NAO WANASEMAJE JUU YA SABATO?
NUKUU.
Katekisimo ya kanisa Katoliki la Roma inasomeka hivi:
Swali: Ipi ndiyo siku ya Sabato?
Jibu: Jumamosi ndiyo siku ya Sabato.
Swali: Kwa nini sisi tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi?
Jibu: Tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa Katoliki …. Liliihamisha ibada toka Jumamosi kwenda Jumapili”.
                Peter Geirmannn, The Convert’s Catechism of Catholic Doctrine (toleo la 1957). Uk. 50.
NUKUU NYINGINE
“Siku ile takatifu, yaani, Sabato, ilibadilishwa kutoka Jumamosi kwenda Jumapili… si kutokana na maagizo yo yote yaliyoonekana katika Maandiko bali kutokana na hisia ya kanisa kwamba linao uwezo wake lenyewe… watu wale wanaofikiri kwamba Maandiko ndiyo yangekuwa mamlaka peke yake, kwa mantiki hiyo, ingewapasa kuwa Waadventista Wasabato , nao wangeitakasa Jumamosi.”-  Cardinal Maida, Askofu Mkuu wa Detroit, Saint Catherine Catholic Church Sentine, Algonac, Michigan, Mei 21, 1995.

“Tunaitunza Jumapili na si Jumamosi kwa sababu Kanisa katoliki lilihamisha utukufu kutoka Jumamosi kwenda Jumapili” Peter Geiermann, CSSR,Doctrinal Catechism, 1957 edition
“Ili makanisa yapate wokovu lazima yatii mamlaka ya Papa na kumkubali kama msemaji wa makanisa Yote ikiwa ni pamoja kupokea muhuli wa uwezo na mamlaka kuifuata Jumapili”
Vatican II ilianzisha Ecumenical movement Makanisa kuwa pamoja yakitii kwa mtu mmoja aliye na muhuri wa mamlaka ya Ukuu wa Kubadili Amri za Mungu kwa sababu Yeye mwenyewe ni Kristu na kukana ukuu wa kuwa Mungu aliumba kwa kutoheshimu kazi ya Siku sita kukiriri kwa maneno kukataa kwa vitendo ili Wanaosema wanaaona watiwe upofu.
Niliposoma kitabu cha The Catholic National, nilipata kujua siri nyingi sana ambazo zilinifanya niendelee kujua haya mambo yamewezekanaje kutokea, nan i kwanini Mungu anayaruhusu, lakini baada ya muda kadiri nilivyokua nikiendelea kufuatilia. Nikalikumbuka neon hili UNABII HAUNABUDI KUTIMIA.
Kitabu hiki kimeandika hivi:-
QUATATION:
”Papa sio mwakilishi wa Yesu tu, lakini ni Yesu mwenyewe,katika mwili”
Source The Catholic National, JULY,1985
UFUNUO 3:18 (MUHURI WA UKUU WA PAPA KUWA NA UWEZO WA KUBADILI AMRI KWA KUWA SI MWAKILISHI TU ILA MWENYEWE NI MUNGU MWENYE MAMLAKA WAO WENYEWE WANASEMA HIVYO SOMA nukuu za Mapapa na UKUU MOJAWAPO NI ILA ZIPO NYINGI)
(Soma Katiba ya Umoja wa Makanisa)
Mama wa makanisa, Ufunuo 17:1-6.

Yamekuwepo maswali na maoni mengi juu ya maagano (AGANO JIPYA NA AGANO LA KALE), wengine wakisema kuwa agano la kale limepitwa na wakati, Sasa tunaokolewa kwa neema tu, pasipo kujua hata maana ya neema, tembelea kwenye uchambuzi juu ya neema ili uweze kukua kiroho.
Lakini pia ningependa kuwauliza watu hawa maswali machache.
NINAOMBA NISAIDIWE MAMBO YAFUATWA KWA UFUPI KABISA HUKU UKITUMIA NUKUU KUTOKA KATIKA BIBLIA,
ni wapi biblia inaonyesha badiliko la sabato kutoka jumamosi (siku ya saba) kwenda siku ya kwanza ya juma (jumapili)
  1.  kama sabato haina maana, je kwa sasa zipo amri tisa na siyo kumi tena?,
  2. Yesu aliposema mkinipenda mtazishika amri zangu alikuwa anamaanisha nini? amri tisa au? naomba maandiko.
  3.  Fungu hili lina maana gani yakobo 2:10. liko agano jipya maana kwako agano la kale ni la mwili.
  4. Kama agano la kale ni la mwilini na agano jipya ni la rohoni, mbona bado mnatumia agano la kale katika mafundisho yenu?
  5. Je mungu atatumia nini kuuhukumu ulimwengu?.
  6.  Je sheria, amria hazina maana mbona mnawatenga wazinzi makanisani mweni.???
  7. Nionyeshe dhambi pasipo sheria.
  8. Mtu anapookolewa kwa neema, huoni akiaacha kusengenya tayari ameitii sheria,
  9.  Biblia inaposema tunaokolewa kwa neema wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu anamaanisha matendo siyo sehemu ya mtu aliyeokoka? 
Kumbuka kwamba sauti ya Bwana ndiyo inayokitangulia kila kitu(1Sam 15:19)  

No comments:

Post a Comment