WAKRISTO NA SIKU ZAO ZA IBADA SURA YA TATU

SURA YA TATU
MTU mmoja alipata kuniambia hivi:-
Unaweza kunidhibitishia kimaandiko kama hii ndio amri kuu?? Je Amri kuu alizotoa Yesu, ambazo ni kama mbili (2 in one) kuhusu upendo mmeiweka wapi hapa??
Nilianza tu kwa kumkumbusha kuwa Yesu alisema sikuja kutangua torati na yesu alitoa Amri kuu ya upendo.

Ni kweli Kuu ni Ya Upendo.
Amri kuu ambayo ni ya Upendo imegawanyika katika sehemu kuu mbili.
a) Upendo kwa Mungu (kumpenda Mungu)
b) Upendo kwa mwanadamu(Kumpenda jirani)

“Sheria yote na Manabii hutegemea amri hizo mbili.” (Mat 22:40)

Mungu ni Pendo ,Na Yesu ni Immanueli (Mungu pamoja nasi), Yesu ni Mungu hivyo utimilifu wa Pendo upo ndani yake ndio maana alitaka tuzishike Amri zake kwa kuweka kipaumbele Upendo si kama mafarisayo ambao walihukumu kwa kupiga wenzao mawe.
a) Mtu aliyetanguliza Upendo kwa Mungu.
b) Upendo kwa wanadamu (jirani) atajikuta amezishika amri zote kumi kwa moyo wote na bila shuruti (maana Yesu huziandika moyoni) “Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, na katika niaa zao nitaziandika” WAEBRANIA 10:16
-Yesu anajua tukimpenda Mungu atakaa ndani yetu na amri zote zitazaliwa na kuandikwa mioyoni mwetu bila kujitegemea wenyewe alitaka kwa Imani.(kumwamini yeye kama mshindi) kuwa ndiye aliyetushindia vikwazo vyote. Tumwamini yeye na kwa kumruhusu atushike mkono na tuwe kama mtoto mdogo Kwenye mikono ya Baba yake. Hii ndio Imani yenyewe. Kisha tutakuwa tumekaandani yake kwa kuwa Yeye ni Pendo,pendo litazaliwa mioyoni mwetu na tutazishika amri zake.

        2Kwa hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu,tumpendapo,Mungu, na kuzishika amri zake.3 KWA MAANA HUKU NDIKO KUMPENDA MUNGU, KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE.” 1 YOHANA 5:2-3.

SOMA PIA
      Laiti wangaliusitawisha moyo wao huu uniogope na kushika amri zangu zote sikuzote, ili mambo yawaendee vema, wao na wana wao mpaka wakati usio na kipimo! (KUMB 5:29)

-Na kama Yesu anasema tumpende Mungu kwa moyo wote na ameshatuambia Kumpenda Mungu ndiko kuzishika amri zake na amri zake tunazijua (KUTOKA 20:1) na Biblia inatuambia “Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi Pendo ndilo utimilifu wa sheria”WARUMI 13:10 neno baya kwa jirani ni lipi? Amri 5-6 hadi 10.

Anazidi kutuambia tunaweza kuyatimiza haya kwa kuyanya mambo yafuatayo;-
 “Usilipize kisasi wala usiwe na kinyongo juu ya wana wa watu wako; nawe mpende mwenzako kama wewe mwenyewe. Mimi ni Yehova.” (Walawi 19:18)

-Ndio maana siku zote joka ametumia mbinu mbalimbali kuanzia mbinguni ambako alipinga utii kwa Mungu na hata aliposhushwa chini akaendeleza Mungu anasema wasile matunda watakufa, Yeye akasema hakika hamtakufa, (MWANZO 2 :17)

SWALI LA UCHUNGUZI:kwa nini baadhi ya watu wengine wengi huheshimu na huabudu hata mizimu kwa kuamini kua bado wale wafu wanaishi? (imetokea wapi Ibada ya hii mizimu, biblia inasema wafu hawajui lolote) Muhubiri anasema mwili huyarudia mavumbi na pumzi humrudia aliyeumba hivyo hili ni danganyo la “hakika hamtakufa” la shetani lili la Mapokeo.
“Kutahiriwa si Kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu” 1 Kor 7:19

Ndio maana siku zote Joka ametumia mbinu mbalimbali kutengua amri za Mungu.
Amri zote za Mungu zilitunzwa na kanisa la mwanzo na kujawa na Roho wa kweli, mpaka miaka ya 300. Pale amri ya nne na kisha ya pili ya Sanamu kuondolewa.

-Baadae amri zote ziliandikiwa katika katika catechism na kuwazuia waumini kusoma biblia. Mpaka leo asilimia 90 ya waumini hufundiswa kutumia Catechism na chuo cha sala na si Biblia maana Biblia ni Nuru isije kuangaza mioyo. Biblia inasema kuwa mwaikataa Amri ya Mungu mpate kuyashika MAPOKEO YENU.( Mk.7:9)

Je, mmesahau fundisho na maonyo yaliyonenwa katika unabii ya kwamba;-
 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”    UFUNUO 22:18 -19
                                                                                                                                                               
Makanisa mengine yakiruhusiwa kufanya namna zao za Ibada bila kukaidi Kukaidi amri ya Mkuu wa makanisa yao .MAANA KWA MANENO YAO WALIMCHAGUA KUWA MSEMAJI WA MAKANISA YOTE YA JUMAPILI KATIKA MKUTANO WA VATICAN. Soma unabii katika Bibliawa mama (kanisa) aliyesema sitakuwa Mkiwa .
(soma Vatican II and liturgy in church union)

1. SWALI LA UCHUNGUZI: KWA NINI NYIMBO ZA MAKANISA YA NEW AGE ZIMEFANANA UKIENDA MAKANISA YA KIROHO JAPO HUONEKANA WAMETOFAUTIANA
2. KWA NINI WACHUNGAJI WENGI HUKWEPA SANA VITABU VYA UFUNUO NA DANIEL?
(SIRI NZITO)
3. KWA NINI WACHUNGAJI WENGI HUCHAGUA AMRI CHACHE TU NA KUZISEMA HUKU WAKIKWEPA KUZUNGUZIA NYINGINE.?(MKUBWA HANYOOSHWEWI KIDOLE) (soma Vatican II and liturgy in church union)

4. KWA NINI SIMON MCHAWI ALIWAONGOZA WAISRAELI KWA MIAKA MINGI TANGU UTOTO WAKE KABLA YA UJIO WA KWANZA WA KRISTO? NA WASIJUE KUWA MCHAWI?

5. KWA NINI JOKA SIKU ZOTE AMEFANYA VITA NA WATU WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU?

joka akamkasirikia Yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda waa Yesu; Ufu 12:17
“Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao amri za Mungu na Imani ya Yesu”
SOMA CATECHISM KATOLIKI (BPNP)TANZANIA 2002 UKURASA 28 KISHA FANANISHA NA AMRI ZA MUNGU KUTOKA 20:1, UANGALIE AMRI HIZI ZIMETOFAUTIANAJE NA MAKANISA MENGINE YAMEZIFUATA ZIPI,NA TAFUTA YAMEKUBALIANA NINI NA VATICAN?

UFUNUO WA YOHANA 14:12
MATENDO YA MITUME 16:4
MATENDO ,, 16:13
MATENDO ,, 13:42

Amri za Mungu Kumi hazikutenguliwa na Yesu Yeye mwenyewe alisema
“…Lakini ukitaka kuingia katika uzima,zishike amri. Akamwambia zipi? Yesu akasema,ni Hizi, Usiue,usiibe,Usishuhudie uongo…….. “Mathayo 19:17

“Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaroga…? Gal 3:1
Ni rahisi sana kwetu kuwashangaa Wagalatia, lakini ukweli ni kwamba mtume Paulo hakuwa anaongea na hao tu, bali sote tutakaokumbwa na roho huyo aliyekuwa amewapagawa kama tunavyowaona watu wengi wa ulimwengu huu. Hamjui ya kuwa “torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo” Gal 3:24.

Unamwamini kristo yupi ?kama hata amri zake hauzishiki, kama torati hutusogeza karibu na kristo JIULIZE NDUGU YANGU WEWE NI KITU GANI KINACHOKUSOGEZA KARIBU NA KRISTO.
Tazama Paulo anavyotushangaa, “Je, mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?” Hii kama si ishara ya kuchanganyikiwa au unafiki au uongo tu wa kawaida ya waongo, ni nini? Wamerogwa!

“Nidhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria” lakini IMANI YAKO IPO WAPI? Kumuamini kristo ni pamoja na kutokutenda dhambi. DHAMBI ni nin basi? DHAMBI NI UVUNJAJI WA SHERIA. KUMBUKA wamwaminio kristo wamefanyika kuwa watoto wa Mungu HAWATENDI DHAMBI(hawavunji sharia za Mungu) “kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” Rum 3:20

Mshahara wa dhambi ni mauti. YAANI ILE LAANA. basi ninyi wenyewe mwaweza kuipima hiyo roho inayowaongoza kuirudia Laana, je, si roho ya kujinyonga hiyo, ile iliyokuwa juu ya Yuda Iskariote???

Maandiko yanatufundisha wazi, kwa jinsi ya rohoni, juu ya kuyashika Maagizo ya Mungu na sheria zake. Unabii unasema vizuri sana, “lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika”. Ndugu zangu hatuwezi kuchukua tu sehemu ya amri za Mungu, na zingine tukaziacha….. ijapo ile iliyokamili, iliyo kwa sehemu itabatilika tu.

Je, mmesahau fundisho na maonyo yaliyonenwa katika unabii ya kwamba;-
 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”  UFUNUO 22:18 -19
                                                                                                                                                             
N:B
Kumbuka amri KUMI za Mungu zipo katika UPENDO KWA MUNGU na UPENDO KWA WANADAMU (JIRANI)

 “KWA MAANA HUKU NDIKO KUMPENDA MUNGU, KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE.”
1 YOHANA 5:2

SOMA MAFUNGU YAFUATAYO. KWENYE BIBLIA BONYEZA HAPA

  1. Yohana 17:17
  2. zaburi 119:142
  3. Mithali 28:9
  4. 1 Yohana 5:3
  5. Isay 66:22.

UBARIKIWE SANA MPENDWA…… ENDELEA KUSOMA SURA INAYOFUATA

No comments:

Post a Comment