Je, Hizi ni
Siku Za Mwisho?
Nabii Daniel alizungumza juu ya “WAKATI WA MWISHO.” Mtume Petro alisema, “katika SIKU ZA MWISHO watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki.” Paulo alisema, “SIKU ZA MWISHO kutakuwako nyakati za hatari.” Wanafunzi wa Kristo walimwuliza juu ya “MWISHO WA ULIMWENGU.” Je, wakati huo umefika? Unaweza kuwa na uhakika?
Mpaka lini Kristo atarudi? Kabla tukio hili kubwa kuliko yote
halijatokea, Biblia huongelea juu ya
kipindi kinachoitwa “siku za mwisho ”— “wakati wa mwisho” — “mwisho
wa ulimwengu [zama]”—“mwisho wa mambo haya” — “mwisho wa siku” — na
ya wakati ambapo historia ya mwanadamu, kama tuijuavyo, “itakapomalizika.”
Bila
shaka, wengi wetu tunaojidai kuwa Wakristo hatuamini-amini katika tukio halisi
la kurudi kwa Yesu Kristo duniani. Wengi tumekua tukijiuliza maswakli mengi
ambayo yametufanya tuwe na shaka juu ya tukio hili ingawa tunaamini-amini
kidogo yaani hatuna uhakka wa kutosha. Hii ni kutokana pia na hali halisi na
mitazamo ya dunia hii.
Miongoni
mwa wanaoamini, wengi wao huamini kwamba inaweza kutokea baada ya miaka mamia
ijayo. Baadhi wanaamini inaweza kuwa “miaka maelfu ijayo.” Wengine kwa namna
fulani wanafikiria juu ya “Har-Magedoni.” Wanahisi kwamba wakati unaweza kuwa
mfupi lakini hawana uwezo wa namna ya KUJUA. Nataka
leo nikuambie kwamba ufalme wa Mungu umekaribi, tena uko karibu mno… ndugu
yangu hizi ni nyakati za mwisho…. Inatubidi kua tayari muda woote.
Hebu tuangalie mitazamo na uelewa wa watu mbalimbali.
Mitume wa Awali Walielewaje?
Mitume wa awali walifikiri kwamba
Kristo angerudi wakati wa maisha yao. Paulo katika 1 Wakorintho 15:51 na 1
Wathesalonike 4:15, alipokuwa akiongelea ufufuo wa wafu utakaotokea Kristo
anaporudi mara ya pili, alitumia neno “sisi” akitegemea
kuwa mmoja wa wale ambao wangekuwa “hai, [tutakao]
salia hata wakati wa kuja kwake Bwana.”
Katika
waraka wake wa pili kwa Wathesalonike, Paulo alikuwa amegundua kwamba hapo
awali alikuwa ameelewa vibaya muda wa kutokea matukio maalumu ambayo ni lazima yatangulie
Kurudi kwa Kristo. Alienda mbele na kuonya dhidi ya wale ambao wangedanganya
wengine juu ya lini tukio hili lingetokea.
Aliandika juu ya “kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo” na ndugu wanapaswa
wawe waangalifu kwamba “Mtu awaye yote
asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu;
akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu”
(2 Wathesalonike 2:1, 3).
Je, unaweza kudanganyika? Hebu tuangalie Kurudi kwa Kristo Mara ya Pili
Je, tuko kwenye siku za mwisho? Kama
ndivyo, unaweza kujua kwa hakika kwamba hii ni
kweli? Yesu alisema kwa wanafunzi wake, “Nitarudi
tena” (Yohana 14:3).
Siku
arobaini baada ya kufufuka kwake, wanaume wawili (malaika) waliwaambia
wanafunzi wake wakati anapaa mbinguni, “Huyu Yesu
aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni”
(Matendo
1:11).
Ndugu
msimaji biblia inatuambia karibu ulimwengu utalifikia tukio la kurudi kwake
kristo kama upeo wa juu kabisa. Tena, je, tunaweza kujua? Mathayo anaandika
maneno ya Kristo: “Maana kama vile umeme
uonekanavyo…ndivyo kutakavyokuwa kuja
kwake Mwana wa Adamu” (Math.
24:27, 30, 37, 39, 42, 44, 46).
Usifanye
kosa! Biblia iko wazi kuhusu Kurudi kwa Yesu Kristo. Mafungu mengi zaidi
yanayoongelea Kurudi Kwake Mara ya Pili duniani yanaweza kunukuliwa.
Kutatokea—na haitegemei juu ya mapendekezo ya wanadamu. Hata hivyo, kabla tukio
hili la juu kabisa halijatokea, mambo mengine mengi zaidi yalisemwa
yatatokea katika kipindi cha kuelekea matukio ya kutisha yanayotangulia kurudi
kwake!
Dhana
ya mwisho wa ulimwengu limekuwa ni somo lenye hisia, kejeli, mjadala, kusisimua
na linalowafanya watu wafikiri kwa miaka 2,000. Bado, ni wachache wanaofahamu
kiasi gani Biblia inaonyesha juu ya kile kinachoweza kueleweka kuhusu
wakati huu.
“Siku na Saa”
Katika
unabii maarufu wa Mlima wa Mizeituni kwenye Mathayo 24, wanafunzi walimwuliza
Kristo, 3“Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja Kwako, na ya mwisho wa dunia?”.
(Mat 24: 3)
Baada ya kujibu swali hili kwa kirefu, mafungu
thelethini-na-tatu baadaye Kristo aliongeza katika fungu la 36 na kusema, 36“Walakini habari ya siku ile na saa
ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke
yake”
(Mat 24: 36)
Je, hii inamaanisha kwamba hatuwezi kujua kiujumla wakati wa Kuja kwa Yesu Mara ya Pili?
Baadhi
wanaamini hivi—na watu hawa hutupilia mbali hitaji lolote la kujishughulisha
ili kujua lini kutakuwa Kurudi kwa Kristo.“Bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,
atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki”?
(Mathayo 24:50-51)
Ni
wazi kwamba karibu kila mmoja hategemei Kurudi kwa Kristo Mara ya Pili katika wakati
sahihi. Ukweli ni kwamba atarudi wakati ambapo wengi hawamtazamii kabisa.
Kwa nini kuna wengi sana ambao hawawezi kutambua kuwasili kwa siku za
mwisho?
Kitu gani kitawafanya wengi wasitambue mwanzo wa tukio hili kubwa?
Kristo
alitoa mfano: “Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na
kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu; nanyi
kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.”
Kristo alitamka kuwa tunaweza kujua “majira” ya Kurudi kwake Mara
ya Pili,
(Maat24: 32-33,)
Ndugu
zangu tsiwe tayari kuridhika bila kujua kile ambacho Biblia inasema unaweza
kujua!
Miaka
mingi iliyopita, kulikuwa na usemi maarufu uliojulikana kama “Ishara za Nyakati”.
Niliufurahia na pengine nawe unaukumbuka. Kichwa hicho kilitolewa kwenye fungu
lingine katika Mathayo. Kwenye sura ya 16, Mafarisayo na Masadukayo walimkabili
Kristo, wakitaka “ishara” kutoka kwake. Aliwaita wanafiki, akisema, “Enyi
wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?
Ingawa
lengo la swali lao lilikuwa kutaka ishara kwamba Yesu alikuwa MASIHI
(angalia Mathayo 12:38-40), mantiki ya Kristo ilikuwa kwamba hawakuweza
kutambua matukio waliyokuwa wakiyashuhudia— “ishara za
nyakati.”
Je, unaweza kutambua ishara za nyakazi ZETU?
Kristo
aliwaambia wanafunzi wake, “Basi mambo
hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa
ukombozi wenu umekaribia” (Luka 21:28). “Mambo” ambayo aliyarejelea
yanajumuisha mfululizo mzima wa matukio yaliyotabiriwa kutokea kwa mara ya
kwanza katika historia! Mambo haya yanatokea—na yanazidi—sasa!
Kuyatazama kwa haraka haraka hakutasaidia. Ni lazima tuchunguze kwa umakini ili
kuweza kuzitambua “ishara za nyakati.”
Mungu
amemtengea mwanadamu miaka 6,000 kujaribu serikali zake mwenyewe, falisafa,
mifumo ya maadili, dini na miundo ya elimu. Fikira za kibinadamu hazitatui na hazina
uwezo wa kumaliza matatizo makubwa ya ulimwengu. Miaka 6,000 ni kama
imemalizika. Na, katika miaka 200 iliyopita au zaidi, ulimwengu umebadilika
sana—na kwa haraka. Matukio yanatokea kwa haraka kwa namna ambayo haijawahi
kuonekana huko nyuma!
Ulimwengu wa Karne ya Ishirini-na-moja
Kila
mmoja anawafahamu watu fulani ambao huzunguka zunguka wakisimama kwenye mitaa
wakipaaza sauti “Tubuni! Mwisho umekaribia!” Kikundi cha filamu cha Holywood kimewaigiza
wengi kati yao. Bila shaka, hakuna mtu anayewajali sana watu kama hao. Lakini
nyakati zimebadilika, na sauti zinazotuambia sasa kuwa mambo hayaendi sawa
zimekuwa nyingi—tena mambo ni mabaya kabisa!
Wazo
la kuwa na serikali moja ya dunia, lilibuniwa ili kuiokoa sayari na mwanadamu
asijiangamize, linasikika mara nyingi zaidi. Hata hivyo, hakuna anayeonekana
kujua namna ya kuunda serikali kama hiyo na kisha kupata ushirikiano wa kila
mmoja ulio wa lazima ili kuifanya ifanikiwe!
Utazame ulimwengu unaokuzunguka. Unaona nini?
Ulimwengu
mzima ulikuwa ni mahali imara mpaka mwanzoni mwa karne ya kumi-na-tisa. Katika
wakati huo maendeleo ya viwanda yalizaa Zama Mpya. Haikuwahi kutokea mpaka
takribani karne moja iliyopita ambapo watu walianza kuendesha magari na kuruka
kwa ndege, na, tangu wakati huo, ustaarabu umekwenda kutoka “Zama za Nyukilia” hadi “Zama za Anga” na ndani ya
muda mfupi chini ya nusu karne umefikia “Zama za
Habari”.
Kuwasili
kwa mavumbuzi mapya, kwa kasi kubwa katika historia, inabadilisha maisha kila
siku. Hebu fikiria matokeo ya viwanda vya uchapaji na utaweza kukubali namna
ambavyo uvumbuzi wa aina moja unavyoweza kuubadilisha ulimwengu. Kompyuta za
kisasa zimefanya yayo hayo—na hakuna kurudi nyuma kwa sababu tu ya uvumbuzi huu
mkubwa. Usafiri wa ndege uliwasili mwishoni mwa karne iliyopita. Japokuwa
makadirio yanatofautiana lakini inasemekana kwamba maarifa ya mwanadamu
yanaongezeka mara dufu kila baada ya miaka michache. Baadhi wanafikiri kuwa
baada ya muda mfupi kasi itaserereka hadi kufikia kila baada ya miezi sita!
Mnamo
mwanzoni mwa miaka ya 1970, Alvin Toffler aliandika kitabu kinachoitwa Fadhaa Ijayo (Future Shock). Kitabu
hiki kikubwa kilielezea aina ya “bumbuwazi la kisaikolojia,” au madhara ya
fadhaa, yatakayowapata watu kwa sababu ya kasi ya mabadiliko katika jamii.
Toffler alidhihirisha kuwa mabadiliko haya yalianza kutokea miaka ya 1970
katika kiwango ambacho watu hawakuweza tena kuyatafakari.
Jamii
ilianza kuingia kwenye kile ambacho Toffler alikielezea kama kuzidiwa—au
“fadhaa.” Alielezea kwamba “yajayo” yalikuwa yanakuwa
“yaliyopo” kwa haraka sana kiasi kwamba watu walianza “kutumia njia za
mkato” namna ile ambayo ustaarabu ulikuwa haujawahi kuona. Miaka michache
baadaye, aliandika kitabu kinachofutia kile cha kwanza kilichoitwa Wimbi la Tatu (The Third Wave). Kitabu
hiki cha pili kilielezea kuongezeka kwa hali hii.
Picha
aliyoielezea haikuwa nzuri, na sasa imekuwa mbaya zaidi!
Wakati
“maendeleo” haya makubwa yakitokea, matatizo ya mwanadamu yamezidi kuwa makubwa
au yasiyotatulika zaidi!
Makadirio
ya ukubwa wa tatizo la UKIMWI yanapitiwa upya mara kwa mara na kuakisi mtazamo
unaotisha zaidi kuliko ilivyofikiriwa hapo kabla. Sehemu nzima za wakazi wa
Afrika zinakadiriwa kufutika kabisa ndani ya miaka michache kwa sababu tu ya
ugonjwa huu mmoja. Lakini pia sio hilo tu bali pia na uwepo wa milipuko
mbalimbali yamagomjwa ya kutisha kama vile EBOLA, MALARIA na mengineyo, yoote
haya yakiiacha Africa katika hali mbaya sana.
Idadi
ya watu duniani inayokadiriwa kuwa bilioni 6.9 (mapema 2009) inaongezeka kwa
kiwango cha 1.2% kila mwaka. Hii ina maana kwamba kufikia mwaka 2050, idadi ya
watu duniani itafikia bilioni 11.1! Makadirio haya yanakuja ingawa kuna ukweli
kwamba magonjwa na njaa vinategemewa kuongezeka zaidi kwenye sehemu za dunia zinazokua
kwa haraka sana! Kuzaliana kwa wingi katika nchi maskini duniani tayari
kumeleta ongezeko hili la watu kama ilivyokadiriwa kutokea.
Sehemu ya Pili bonyeza HAPA
by Fortune akilimali.
Sehemu ya Pili bonyeza HAPA
by Fortune akilimali.
No comments:
Post a Comment