SURA YA 3
KIBALI CHO CHOTE CHA
UTAKATIFU WA JUMAPILI
JE KUNA KIBALI CHA
MUNGU KWA BADILIKO HILI?
Kwanza kabisa
inatupasa sote kufahamu kuwa maandiko ni neon la Mungu mwenyewe kama Biblia
yenyewe inavyotuambia ya kwamba iliandikwa chini ya
uvuvio wake Mungu, na kamwe haijikanushi
yenyewe “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu”
(2 Timotheo 3:16).
Yesu Kristo
hakubadili Sabato. Yeye kama Muumbaji aliifanya ili iendelee kuwako.
“Msidhani ya kuwa
nalikuja kuitangua torati [sheria] au manabii; la, sikuja kutangua, bali
kutimiliza”
(Mathayo 5:17).
KATIKA kipindi
choote kabla na baada ya kristo, Wanafunzi wake Kristo na makanisa yale ya
kwanza ya Kikristo hawakupata kusikia kitu kama hicho cha badiliko lililofanywa
na Mungu kuhusu utunzaji wa Sabato. Kwa hiyo,utunzaji wa siku nyingine yo
yote kama Sabato mbali na ule wa siku ya saba hautambulikani katika Agano
Jipya.
Ni dhahiri kwamba
hakuna sehemu ndogo hata moja ya mahubiri Yake Kristo ambayo haionyeshi kitu
gani ni halali na cha haki kutendwa katika siku ile ya saba, jambo ambalo ni
gumu sana kulieleza kwa wale wanaodai kwamba wanasadiki [Kristo] aliitangua
Sabato.
Ila kulikua na
tofauti kati ya sharia za Sabato waliokua wakiishikilia wayahudi ambayo ilikua
ni mzigo kwao na Sabato halisi ambayo Kristo alikua akiitunza. Utunzaji wa
Sabato wa Wayahudi wa siku zile za Kristo ulikuwa haufanani kabisa na uleambao
Mungu alikusudia.
Shetani alikuwa
amefanya kila aliloweza kwa njia ya majaribu yake yapotoshayo kuwafanya.
Wayahudi waache kuitunza Sabato. Katika jambo hilo alifanikiwa kwa sehemu
tu. Mungu akawaacha watu wake kwenda utumwani kule Babeli kwa sababu ya
dhambi zao, ambazo zilikuwa ni pamoja na kuivunja Sabato. Mara tu waliporudi
toka utumwani, Wayahudi hao waliazimu kuitunza Sabato kwa uaminifu sana
kama Mungu alivyoamuru kwa kuziweka sharia kali juu ya mtu yeyote atakayeivunja
Sabato ambazo ziliwafanya wawe watumwa wa sheria.
Mbinu hii ya Siku ya
Sabato kujazwa na masharti mengi yaliyokuwa mzigo mzito uliowalemea watu ilikua
ni mbinu pekee ya shetani kuwafanya watu waendelee kuichukia siku hiyo ya
Sabato.
Yesu alipojitokeza
kama Mwalimu wa watu miongoni mwa Wayahudi, Alilitumia kila tukio kuiweka huru
siku hiyo mbali na sheria zile zilizotungwa na wanadamu ambazo zilikuwa mzigo
mzito uliowalemea watu.
MIUJIZA SIKU YA
SABATO
Naam, alizitumia
vizuri nafasi hizo, maana kwa makusudi mazima aliichagua Sabato kama siku ya
kufanya miujiza Yake mingi pamoja na matendo yake ya huruma.
Akiwa ndani ya
sinagogi siku ile ya Sabato, alimtoa "roho ya pepo mchafu" kutoka
ndani ya mtu yule aliyekuwa amefungwa na pepo huyo. Baadaye, Sabato ile ile,
alimponya "homa kali" yule "[mkwewe Simoni], mamaye mkewe."
(Angalia Luka 4:30-39.).
Hata hivyo, Yesu
aliendelea tu kuyasahihisha mawazo yao kuhusu nini kilichofanya utunzaji wa
Sabato uwe sahihi, naye aliendelea kufanya matengenezo katika utunzaji wa
Sabato kwa kuwa "Mwana wa Adamu ndiye Bwana [Yehova] wa Sabato."
(Mathayo 12:1-8.).
Vitabu vinne vya
Injili huitaja siku ya kwanza ya juma mara sita, na katika mafungu hayo wale
wanaoitunza siku ya kwanza ni lazima wakipate kibali chao kwa utunzaji kama
huo. Vifungu vinavyoitaja siku ya kwanza katika Injili ni hivi:
a.
Mathayo 28:1
b.
Marko 16:1,2,9;
c.
Luka 23:56 na 24:1;
d.
Yohana 20:1,19.;
Ukivichunguza
vifungu hivi kwa makini utagundua mambo yafuatayo:-
- Yanasema juu ya Sabato, ni kweli, lakini yanaainisha[yanatofautisha] kwa uangalifu mkubwa sana kati ya Sabato na siku ya kwanza ya juma, yakiliweka wazi jambo hili kwamba Sabato ya Agano J ipya ni siku ile iliyo kabla ya siku ya kwanza.
- Inadhihirika kwamba hayasemi kitu cho chote juu ya badiliko la Sabato.
- Hayatoi cheo [sifa] cho chote cha utakatifu kwa siku ile ya kwanza.
- Yanatoa cheo [sifa] hicho kwa siku ile ya Saba.
- Hayasemi kwamba Kristo alistarehe siku ile ya kwanza, jambo ambalo lingekuwa la lazima katika kuifanya siku hiyo kuwa Sabato.
- Hayasemi lo lote kuhusu baraka yo yote kuwekwa juu ya siku ile ya kwanza.
- Hayatuambii lo lote juu ya Kristo kwamba kuna wakati wo wote aliopata kusema neno lo lote kuhusu siku ya kwanza, aidha kama ni siku takatifu, au vinginevyo.
- Hayatoi kanuni au amri yo yote kuhusu utunzaji wake [siku ya kwanza].
- Hakuna cho chote katika mafungu haya kinachotangaza kuwa siku ya kwanza iangaliwe na wafuasi wake Kristo kama kitu cho chote kile zaidi tu ya kuwa ni siku ya juma ya kawaida kama inavyotajwa ----- ni "siku ya kwanza ya juma" tu.
Mungu anasema kwamba
Sabato ni “agano la milele” na ya kwamba ni “ishara kati ya mimi na wana wa
Israeli milele” (Kutoka 31:16,17).
Jiulize ndugu yangu
ni nani aliyeipa cheo na mamlaka ya kuheshimiwa na amri ya kutuzwa siku hiyo ya
kwanza?
Endelea kufuatilia
makala hizi utaona ni jinsi gani, wakati gani, na nani aliyebadili majira haya
na amri juu ya Sabato ya Bwana.
JE! KUNA VITABU
VINGINE KATIKA BIBLIA VINAVYOONYESHA KUTAJWA KWA SIKU YA KWANZA NA KUTOA KIBALI
CHA KUABUDU KATIKA SIKU HIYO?
KUTAJWA KWA SIKU YA
KWANZA KATIAKA VITABU VINGINE VYA BIBLIA
Baada ya
kuyatafakari kikamilifu mafungu yote haya, Kamusi ya Biblia iliyoandikwa na
Smith, katika makala yake juu ya "Siku ya Bwana," anakiri kama
ifuatavyo:
LICHA ya vitabu vya
injili Siku ya kwanza ya juma imetajwa katika sehemu nyingine. Ya kwanza kati
ya hizo imo katika kitabu cha Matendo ya Mitume:
"Hata siku ya
kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu,
akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa
manane. Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika"
(Mdo 20:7,8).
Kifungu
hiki hakina ushahidi wo wote kuhusu badiliko la Sabato, wala hakiungi mkono
wazo la utakatifu wa siku ya Jumapili. Ulikuwa ni mkutano uliofanyika siku ya
kwanza ya juma, lakini sio mkutano wa ibada ya kawaida ya siku ya
Jumapili. Ulifanyika usiku. "Palikuwa na taa nyingi," na Paulo
"akafuliza maneno yake hata usiku wa manane."
KABLA ya kuendelea
kukichambua kifungu hiki, ni lazima kuchunguza katika biblia NI WAKATI GANI
SIKU HUANZA na NI WAKATI GANI SIKU HUISHA.
Siku
za Biblia zinaanza na kuisha jua linapozama [machweo]. Siku ya kwanza ya
Biblia huanza jua linapokuchwa [machweo] Jumamosi jioni, na inakwisha jua
linapokuchwa Jumapili jioni. Kwa hiyo, "usiku wa manane" ambao
Paulo "alifuliza maneno yake" ni lazima ungekuwa, ungaliweza tu
kuwa, ni ule wa Jumamosi usiku.
Ni dhahiri kuwa
Mtume Paulo kama aligeuza siku hii na kuifanya jumapili siku ya ibada angekua
ameivuna sharia ya Mungu, “Dhambi ni uvunjaji wa Sheria [Amri
Kumi]”
(1
Yohana 3:4)
Hebu turejee vitabu
vifuatavyo:-
Conybeare na Howson,
katika kitabu chao cha 'LIFEAND EPISTLES OF THE APOSTLE PAUL,' wakishughulika
na suala la wakati mkutano huo ulipofanyika, wanasema maneno haya:
"Ilikuwa ni
jioni ile iliyokuja baada ya Sabato ya Wayahudi. Jumapili asubuhi merikebu
ilikuwa tayari kwa safari." ----- (Scribner's ed., Vol.II, uk.206.)
Daktari [Dkt.] Horatio B. Hackett, profesa wa Agano Jipya la Kiyunani
[Kigiriki] katika Chuo cha Thiolojia cha Rochester, katika kitabu chake cha
'COMMENTARY ON ACTS,' asema hivi:
"Wayahudi
walihesabu siku zao toka jioni hata asubuhi, na kwa kanuni ile usiku ule wa
siku ya kwanza ya juma ungekuwa sawa na usiku wetu wa Jumamosi. Endapo Luka
alihesabu hivyo hapa, kama wengi wanaotoa ufafanuzi wao wanavyodhani, basi,
mtume alingoja mpaka Sabato ya Wayahudi ilipokwisha, na kufanya mkutano wake wa
kidini wa mwisho [wa kuagana] pamoja na ndugu zake kule Troa... Jumamosi usiku,
naye hatimaye aliendelea na safari yake
Jumapili
asubuhi." ----- (Toleo la l882, uk.22l,222.)
Ahsante Mungu akubariki.
No comments:
Post a Comment