KUENEA KWA DESTURI ZA KIBABELI ULIMWENGUNI KOTE
Ibada ya sanamu ikiwemo desturi yao
ya sala za kujirudiarudia ilisambaa na kuenea duniani kote, mfano mzuri was ala
na namna hii zinaonekana huko Efeso. “Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni
myahudi, wakapiga kelele wote kwa pamoja kwa muda wa kama saa mbili wakisema,
Artemi wa Waefeso ni mkuu”
(Mdo 19:34).
Mfumo huu wa sala ya kujurudiarudia
ulionekana kushamiri sehemu mbalimbali katika uso wa dunia. Sheria kali
ziliwekwa kwaajili ya mtu yeyote atakayepinga na kuidharau miungu yao.
Ni dhahiri kwamba mfumo wa sala hizi
uliambatana na shanga ambazo zilikua zikihesabiwa wakati wa sala zao za
kiagani. Vilevle mfumo huu wa shanga unaonekana kushamiri pia katika nyakati
hizi,
Huko india Wabudha wanatumia shanga zao
ambazo zinayohesabiwa wakati wa sala, na mfumo was ala zao ni wa kujirudiarudia
pia.
Waislamu nao wana tumia mfumo huu wa
shanga iitwayoTashibi, inayohesabiwa wakati was ala zao za kujirudiarudia.
Halikadhalika Waroma nao wanatumia
aina hii ya shanga/mkufu iitwayo Rozari,
yenye pingili ‘55’ huhesabiwa pia wakati wa kusali na mfumo wa sala zao ni wa
kujurudirudia.
Wakati wamisionari wanatembelea, nchi
za kaskazini mwa dunia, ambako huko jua lilikua likichomoza maramoja kwa wiki, na
kutokana na kwamba ibada hizi za kipagani zilikua zimekwisha kuenea, waliwakuta
watu wakiabudu siiku ili jua lilipokua likionekana, kama ishara ya kumuenzi
mungu jua,
Wamisionari walishindwa kubadilisha
mfumo ule wa kuabudua na kwa sababu ilikua ni desturi yao kuabudu katika siku
ile, ilibidi na wao waitumie siku ile kutoa mafundisho yao, siku hiyo ya
kuabudu mungu jua ilijulikana kama “SUN
DAY”. Ambapo baadaye ikawa ndiyo siku iliyozoeleka na kuitwa “SUNDAY”.
Wamisionari hao walipofika pwani ya Afrka
Mashariki, waliwakuta Waswahili wakivua na kula visamaki vidogo, Wamisionary
hao walivipenda sana visamaki vidogo kwa kuwa vilifanana na moja ya miungu yao,
mungu samaki aliyejulikana kama “DAGON”. Wakawa wanaviita DAG, DAG,DAG
waswahili wa pwani ya Africa ya masharki wakaviita “Dagaa”.
Kama utakumbuka katika kitabu cha
Samweli, wakati
“2Wafilisi wakalichukua
sanduku,la Mungu, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na
Dagoni.” (1 Sam. 5:2.)
Moja ya miungu Wafilisti Waliokua
wakiiabudu ni DAGON “mungu samaki” kama utaweza kufuatilia ni jinsi gani
walivyokua wakimwabudu na kumpa utukufu mwingi wakidhani ya kuwa ndiye mungu
wao Muumbaji.
Picha ya Dagon.
Hii ilitokea wakati Wafilisti walipoliteka
Sanduku la Agano, nakwenda kuliweka kwenye nyumba ya DAGON, ilipofika subuhi ya
siku ya pili, walishangaa sana kumkuta Dagon ameanguka kifudifudi, akilisujudia
Sanduku la Agano la Mungu. Biblia inaeleza vizuri habari za Dagon katika kitabu
cha Samweli wa kwanza.
Na watu wa Ashdodi walipoamka
alfajiri siku ya pili, Kumbe! Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya
sanduku la bwana. Wakaitwaa Dagoni wakairudisha mahali pake tena.
Chakushangaza zaidi kwa watu hawa wa
Ashdodi walipoamka tena asubuhi ya siku inayofuata wakamkuta tena mungu wao
Dagoni amenguka kifudifudi mbele ya sanduku la Bwana, wakati huu hali ya Dagoni
ilikua mbaya zaidi kwani alikua amevunjika kichwa na vitanga vya mikono yake,
akabakia kiwiliwilwi tu.
“4Hata walipoamka kesho yake asubuhi, Kumbe! Dagoni ameanguka
chini kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA, na kichwa chake Dagon na vitanga
vya mikono yake vyote viwili vimekatika, vipo vimelala kizingitini; Dagoni
akasalia kiwiliwili chake tu. Kwa hiyo makuhani wa Dagoni na mtu awaye yote aingiaye
nyumbani mwa Dagoni hawakanyagi kizingiti cha nyumbani mwa Dagoni huko Ashdodi,
hata leo.” (1 Sam. 5:4,5)
Matukio yoote haya yalikua ni
kithibitisho cha kutosha kuwainesha wafilisti kuwa yuko Mungu mwenye nguvu
kuliko yule mungu wao waliokua wakimtegemea na kudhani kuwa ndiye mwenyenguvu
ambaye anaweza kuwasaidia.
Tunaona katika kitabu waamuzi jinsi
Wafilisti walivyokua wakimtumainia mungu wao Dagon na kuamini kua hakika yeye
ndiye alikua mweyenye nguvu kuliko miungu wengine
“23Kisha wakuu wa Wafilisti
wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana
walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui yetu mikononi mwetu. 24Na
watu walipo mwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia
mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi
miongoni mwetu” ( Waamuzi 16:23-24)
UNABII WA DANIEL
Mungu anayefunua siri.
Baada ya dola ya Warumi kuvunjika katika karne ya 5 B. K.
Haikufuatiwa na dola nyingine yoyote kuu, na kwa kweli haijakuwapo dola ya tano
ya kulinganishwa kimamlaka, pamoja na kuwepo jitihada kubwa za watu wenye tamaa
kuunda nyingine.
Maeneo ya dola ya Kirumi yalimeguka
kutokanana uvamizi wa makabila jeuri ya Kihan, Kigoti, Kivisigoti na Kivandali,
yaliyoanzisha tawala zao wenyewe tofauti. Mataifa ya sasa ya Ulaya yametokana na falme hizo.
Katika kipindi chote cha historia ya miaka 1500 mpaka sasa, mataifa hayo yamebakia
katika mgawanyiko, kama ilivyoashiriwa na nyayo za ile sanamu –nusu chuma na
nusu udongo: “ nusu una nguvu, na nusu yake umevunjika … hawatashikamana.“
(Dan. 2:42-43)
KWA kuwa yupo Mungu anayefunua siri.
Kama ilnsvyoelezwa katika kifungu hiki:-
“Yupo Mungu mbinguni
afunuaye siri.. Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye,
na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.” (Ms. 28,45)
Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akiwa
amejaa kujikinai na ufahari, aliona katika ndoto sanamu moja kubwa sana ya mtu, yenye sehemu tano (tazama uk. 16,17):
Kichwa cha sanamu kilikuwa cha
dhahabu.
Kifua chake na mikono kilikuwa cha
fedha.
Tumbo lake na mapaja lilikuwa la
shaba.
Miguu yake miwili ilikuwa ya Chuma.
Lakini nyayo na vidole zilikuwa
mchanganyiko wa chuma na udongo wa mfinyanzi.
Kisha jiwe likatokeza ‘lililokatwa
kutoka mlimani bila kazi ya mikono.’ Likaangukia nyayo za sanamu ile, likaiangusha
yote chini, na kuzisaga sehemu zake kuwa unga, kiasi kwamba upepo ukaupeperushia
mbali. Baada ya hapa lile jiwe likakuakuwa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.
Nebukadreza alisumbuliwa sana na
hatima ya sanamu ile, kwa sababu hakuna kati ya watu wake wajuzi aliyeweza kumwambia
ilikuwa na maana gani. lakini Daniel, nabii wa Israel alimwambia “kuna
Mungu mbinguni afunuayesiri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa
siku za mwisho “ (Dan. 2:28).
Nabii Daniel alielezea maana ya sanamu ile.
“Kichwa cha dhahabu kiliwakilisha utawala wa Nebukadreza mwenyewe. Ulikuwa
ufuatiwe na mwingine, wa hali ya chini zaidi (kifua na mikono ya fedha); na
baada ya huo wa tatu (wa shaba); alafu wa nne (miguu ya chuma) ambao ungekuwa
na nguvu na kishindo, lakini nyayo na vidole viliwakilisha falme
zilizogawanyika, nusu nguvu na nusu dhaifu”. (Ms.
37 –42)
NDOTO YA MAANA SANA
Wakati akitafakari mambo
haya na akishangaa kama ufalme wake ungedumu milele, Nebukadneza alilala
usingizi. Usiku ule alikuwa na ndoto ya maana, lakini alipoamka alikuwa hawezi
kukumbuka kitu chochote. Alihisi hata hivyo, kuwa hii ndoto kwa namna fulani
ilikuwa na majibu kwa swali lake juu ya mambo ya baadaye.
Mara moja Nebukadneza
aliwaita wenye hekima katika utawala wake kumsaidia akumbuke ndoto yake haijalishi
ni kiasi gani cha umizimu wao, unajimu, uchawi, au ulozi walihitaji kutumia.
Wenye hekima walikusanywa, lakini hawakuweza, kupitia elimu ya mambo yote haya,
kufunua ndoto ya mfalme.
Akiwatambua hawa wenye hekima kuwa walikuwa
wadanganyifu na kuwa wasingemsaidia, mfalme alikasirika na kuamuru wakamatwe na
kuwekwa kizuizini wakisubiri kuuawa. Danieli na wenzake walidhaniwa kuwa wenye
hekima, lakini hawakuitwa au kuwepo mbele ya mfalme. Hata hivyo, bado
walijumuishwa katika kukamatwa wenye hekima kwa kijumla.
Danieli alikata rufaa ili
hatua hii ya kuuawa icheleweshwe, akiahidi kuwa baada ya muda mfupi angempatia
mfalme habari alizokuwa anazitaka. Usiku ule yeye pamoja na wenzake waliweka
ombi lao kwa bidii mbele za Mungu ili kujua ndoto ya mfalme na tafsiri yake.
Walijua kwamba Mungu huwaheshimu wale wanaoweka tumaini lao lote kwake, na kwa
hiyo walienda kulala wakiamini kwamba Mungu angefanya mapenzi yake yatimie.
Usiku ule Mungu kwa rehema alifunua ndoto ya mfalme kwa Danieli, na hali
kadhalika ilichomaanisha, hivyo ikionyesha kwamba Mungu pekee anajua ya
mbeleni.
SURA YA SANAMU YA FALME
Ndoto hii ya maana ilikuwa
juu ya sanamu kubwa ambayo kichwa chake kilikuwa cha dhahabu. Kifua chake na
mikono vilikuwa vya shaba. Miguu yake ilikuwa chuma, na nyayo zake na vidole
vyake [pia] vilikuwa mchanganyiko wa chuma na udongo (angalia Danieli 2:28-33).
Kichwa cha dhahabu
kilitafsiriwa wazi wazi kuwakilisha Babeli (angalia Danieli 2:37-38). Chini ya
Nebukadneza, Babeli ilikuwa imekusanya dhahabu kutoka katika mataifa yote
iliyoyateka, [dhahabu hii] ikiifanya kuwa taifa tajiri sana la zamani.
Lakini hiyo haiko katika
ukuu wa utajiri unaodhaniwa, au katika hali ya kutoonekana ambayo mataifa au
watu wanaweza kupata nguvu, bali katika kujua na kutimiza mapenzi ya Mungu. Na
hatima yao inaamuriwa na mtizamo wao kwa makusudi ya Mungu kwao.
Ufalme wa Nebukadneza uliishia
tu wakati wa utawala wa mjukuu wake Belshaza, wakati taifa la pili,
lililowakilishwa kwa kifua na mikono ya shaba, lilipongia katika uwanja wa
kutawala. Kwa ujumla, ni ufalme ulio hodari zaidi ambao unashinda ule ulio
dhaifu, lakini unabii unaonyesha kwamba hii isingekuwa utaratibu wa mambo
(angalia Danieli 2:39).
Katika sanamu, historia ya
mataifa iliendelea kuanzia kwenye kichwa hadi kwenye miguu, na kila badiliko
liliakisiwa kwa madini dhaifu yakilinganishwa na yale ya taifa lililotangulia.
BABELI YAANGUKA
Majeshi shirikisho ya
Waamedi na Waajemi yaliushambulia na kuushinda ufalme wa Babeli, kumwua
Belshaza--mfalme wa mwisho wa Babeli, na kisha Dario Mmedi alitawala katika
sehemu yake (Angalia Danieli 5:28-31).
Zaidi ya karne moja kabla,
Bwana alikuwa amefunua kupitia Isaya mbinu ambayo kwayo Babeli ingechukuliwa na
mtu ambaye kupitia uongozi wake jambo hili lingetokea
(Angalia Isaya 44:27-28; 45:1-2).
Chini ya uongozi wa
Koreshi Mwajemi, majeshi ya Waamedi na Waajemi, yaliweza kubadilisha mkondo wa
maji ya Mto Frati kwa muda kidogo. Wakati wa kipindi hiki waliingia mjini kwa
kutumia njia ya maji ambayo waliyakausha. Hata juhudi zao zisingekuwa na maana,
kama malango ya shaba yasingekuwa yameachwa wazi, bila kulindwa na walinzi
wanaotetea [ufalme], wakati mfalme na wakuu wake walisherekea na kunywa (Angalia Danieli 5).
Kama tu fedha ilivyo
dhaifu kwa dhahabu kithamani, basi Waamedi--Waajemi walikuwa dhaifu kwa utajiri
na anasa. Wakati Himaya ya Waamedi--Waajemi ilikuwa na nguvu katika mambo ya
vita na eneo walilokalia, haikuweza kuizidi Babeli katika kujilimbikizia
utajiri au elimu. Himaya ya Waamedi/Waajemi ilikuwepo kwa karibu miaka mia
mbili, kuanzia 539 KK hadi 331 KK.
Ufalme uliofuata, ule wa
shaba, ungewakilisha hatimaye ufalme ulioiangusha Uajemi. Tunajua kutokana na
historia kwamba ilikuwa ni Wayunani, chini ya Alexander Mkuu, ambaye katika
mapigano matatu ya nguvu (Granicus, mwaka 334 KK; Issus, mwaka 333 KK; na
Arbela, mwaka 331 KK) aliyashinda majeshi ya Waajemi, akiifanya Uyunani Himaya
ya baadaye.
Ukweli huu wa kihistoria
unaonyeshwa pia waziwazi katika njozi nyingine na Danieli, ulioko kwenye
kumbukumbu katika sura ya 8, ambapo inaelezwa ufalme wa kuwashinda Waajemi
ungekuwa Uyunani (Angalia Danieli 8:2-8,
20-21).
Shaba yalikuwa ni madini
yaliyotumiwa na Wayunani kote, na pia yaliletwa katika utengenezaji wa silaha
na vyombo vya vita.
Roma, ambayo iliwakilishwa
na miguu ya chuma, iliyashinda majeshi ya Kiyunani katika vita vya Pydna mwaka
168 KK. Roma hatimaye ilitawala ulimwengu kutoka mwaka 168 KK hadi 476 BK,
wakati ilipoanguka mwishoni kwa makabila ya kivamizi ya washenzi.
Kwa zaidi ya miaka 500,
Roma ilionekana kuwa isingeshindwa. Bendera zake zilipepea kutoka visiwa vya
Uingereza mpaka mto Frati, Kutoka Bahari ya Kaskazini mpaka Jangwa la Sahara.
Makaisari wake waliabudiwa kama miungu, na kwa uwezo wake ilifanya ulimwengu wote
kama nyumba moja ya kifungo. Katika maneno ya mwanahistoria Edward Gibbon, “Kupinga
ilikuwa ni hatari ya kifo, na isingewezekana kuruka.” The Decline and
Fall of the Roman Empire, gombo la 1, ukr. 190.
Wakati Roma ilipoanguka,
eneo lake liligawanywa katika sehemu kumi ambazo sasa zinafanya mataifa ya
Ulaya. Kama ambavyo chuma na udongo kwa sehemu vina nguvu na kwa sehemu dhaifu,
kwa hiyo ndivyo ingekuwa kwa mataifa haya kumi ya Ulaya ambayo nyayo na vidole
vyake vya sanamu hii ilichowakilisha. Kama ambavyo chuma na udongo haviwezi
kuchanganyika au kushikamana, kwa hiyo mataifa haya yenyewe yasingeungana kama
dola ya mamlaka inayotawala ulimwengu.
Kwa karne kumi na tatu za
mwisho, watu wenye nguvu wametafuta kuhuisha utukufu wa Himaya ya Kirumi ya zamani,
wakiunganisha pamoja mataifa mbalimbali ya Ulaya. Tukianza na Charlemagne na
kuendelea na Charles V, Louis XIV, Napoleon, Kaiser William II, na Adolph
Hitler--wote kwa ishara wameshindwa, japo kwa wakati lengo lilionekana
kufikiwa. Maneno saba madogo ya unabii yalisimama katika njia yao:
“Hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo” Danieli 2:43. Na mataifa ya Ulaya, moja moja au yote,
hayatashikamana katika mamlaka ya kutawala ulimwengu tena!
NDOTO BADO HAIJATIMIZWA
Lakini hii haikuwa mwisho
wa ndoto. Pia ilifunuliwa kwamba katika siku za falme hizi, Mungu wa mbinguni
atasimamisha Ufalme wake wa milele. Ufalme huu wa haki, uliowakilishwa na jiwe
[mwamba] ambalo liligonga sanamu miguu yake, ungeendelea kukua mpaka dunia yote
ijazwe, na hakuna hata mamlaka moja ya dunia ambayo ingezuia (Angalia Danieli 2:34-35, 44).
Ingawa wafalme wengi na
mamlaka zimejaribu kumharibu Kristo--aliyewakilishwa na Jiwe, na wameendesha
vita dhidi ya wafuasi wa ufalme wa Kristo wa haki, bado hakuna hata [ufalme
mmoja] uliofanikiwa na wala hakuna utakaofanikiwa. (Angalia 1 Wakorintho 10:4)
Kristo na ufalme wake
utatawala milele, utukufu wake na kweli utafunika na kuijaza dunia hii kama tu
maji yaijazavyo bahari Na mataifa yote maovu ya dunia yatasagwasagwa kama unga
wakati Kristo--Mwamba anapokuja tena katika mawingu ya mbinguni.
BADO KUNA MUDA WA KUANGUKA
KWENYE JIWE
Rafiki, je utakuja kwa
Kristo leo, ukianguka juu ya Mwamba huu wenye nguvu na kuvunjika katika moyo,
ukitubu dhambi zako zote upate kuinuka na kuishi maisha mapya ukiwa na nafasi
ya kuwa na uzima wa milele ikiwa utakuwa mwaminifu hadi mwisho?
Au utabaki na majivuno na
kutotubu, uking’ang’ania kwenye dhambi zako utakapokuwa umechelewa, na
kukutikana na Mwamba huu wa nguvu ukikuangukia na kukusaga mpaka kuwa
vumbi--bila nafasi ya uzima wa milele?
Ndugu msomaji, je unataka
kungukiwa na Mwamba huu mkuu na kupotea? Au unataka kupata hifadhi na kujificha
katika Mwamba huu na kuokolewa? Uchaguzi ni wako.
“Ee Mungu, ukisikie kilio
changu, Uyasikilize maombi yangu. Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia
moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio
langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate.” (Zaburi 61:1-3.)
“Ingia
ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa BWANA, mbele ya
utukufu wa enzi yake.”
(Isaya
2:10.)
“Nimekukimbilia
Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye, uniopoe, Unitegee sikio
lako, uniokoe. Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Nitakakokwenda siku zote.
Umeamuru niokolewe, Ndiwe genge langu na ngome yangu.”
(Zaburi
71:1-3.)
“Wote anipao Baba watakuja
kwangu; wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.”
(Yohana
6:37)
No comments:
Post a Comment