SEHEMU YA
KWANZA
WAKRISTO WA
AWALI KABLA YA GHARIKA
Zamani wakati wafuasi wa Kristo
wakiieneza Injili ya Yesu Kristo, wapagani waliona kuwa, adui dhidi ya Mkombozi
angedhihirishwa kwa wote ambao wangeliamini jina lake.
mbali: kwa hiyo, moto wa mateso dhidi
ya wakristo iliwashwa. Ghafla wakristo wakanyanganywa mali zao na kuondolewa
katka nyumba zao. Watu wingi; waungwana na watumwa; matajiri kwa masikini;
wenye elimu na wasio na elimu, wakauawa bila Upagani uliona kuwa kama Injili
ingeshinda,mahekalu na madhabahu yake yangefutiliwa huruma.
Hapo ndipo walipoyakumbuka maeno ya
Yesu Kristo aliyowaeleza wanafunzi wake,”9Wakati
huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakua watu wa
kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu 21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo
dhiki kubwa ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa,
wala haitauwapo kamwe.”(Mat.24:9,21).
Tangu wakati wa nero mateso
yaliendelea kwa karne kadhaa, wakristo walisingiziwa kuwa vyanzo vya njaa maafa na matetemeko. Watoa habari walikua
tayari kulipwa ili kutetea udanganyifu kua wakristo ni waovu.
Wakristo walizidi kuvumilia na
kuendelea kuitetea imani yao, wakiyakumbuka maneno ya Yesu na ahadi zake kwa
watakaokua washindi; lakini wakijua kuwa sikuhizo ni chache na zimekwisha
fupizwa kwa ajili ya wateule..”Na kama siku hizo zisingalifupizwa,
asingeliokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo”.(Mat.24:22).
Lakini pia maneno ya Yesu yalizidi
kuwatia nguvu wakijua ya kuwa tuzo yao ni kubwa mbinguni, kwani ndivyo manabii
walivyoteswa kabla yao.”11Heri ninyi watakapowashutumu
na kuwaudhi na kuwanenea kila neon baya kwa oungo, kwa ajili yangu12
Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni”(Mat
5:11,12).
Kwa imani walimwona kristo na malika
wakiwaangalia kwa shauku kubwa na kuheshimu uthabiti waona kuukubali. Sauti
ilikuja kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu ”10Uwe
mwamnifu hata kufa, name nitakupa taji ya uzima.”(Uf.2:10)
Juhudi za shetani za kuangamiza
kanisa la Mungu kwa vurugu hazikusaidia. Watendakazi wa Mungu waliuawa na
injili ilizidikuenea na wafuasi wa kristo walizidi kuongezeka mara dufu,
mkristo mmoja alisema “Kadiri mnavyotufyeka, ndivyo tunavyoongezeka;
damu ya Wakristo ni mbegu”
Mipango ya shetani ya kupambana na
Mungu kwa ufanisi iliwekwa kwa kupandisha bendera zake katika kanisa la
Wakristo ili akipate kile alichokikosa, mateso yakakoma. Badala yake kukawa na
vishawishi vya mafanikio na heshima ya kidunia
Waabudu sanamu walipewa kupokea
sehemu ya imani ya Kikristo. Walidai kuwa wamempokea Kristo lakini walikua
hawjashawishikaa kuwa ni wenye dhambi, na hawakua hawajaona haja ya toba wala
badiliko la moyo.
Uongo dhidi ya ukweli uliendelea na mpango
wa shetani wa kuwayumbisha na kuwapoteza wana wa Mungu uliendelea kama
ilivyoonyeshwa kwenye sura inayofuata.
No comments:
Post a Comment