KUZALIWA UPYA KIROHO
MAANA YA UBATIZO
“Basi
tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama kristo
alivyofufuka katika wafu kwa njia ya
utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana
kama tulivyounganika naye katika mfan wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa
mfano wa kuunganika naye; tukijua nano hili, ya kuwa utu wetu wa kale
ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi
tena”. Rum 6:4-6.
Ubatizo huonyesha mambo muhumu
matatu:-
Kuifia dhambi.
Kuzaliwa upya katika Kristo.
Kumpokea Kristo molele.
Ubatizo ni lazima uendane na imani ya
kweli. Maana wote wenye imani ya kweli ni watoto wa Mungu,
1Yoh. 5:4. “Kwa maana kilichozaliwa na Mungu
huushinda ulimwengu; na huko ndiko kuushinda ulimwengu, hiyo imani yetu”.
Vivyo hivyo ubatizo huambatana na
imani biblia inasema kuwa mtu ni lazima aamini ndio kasha abatizwe, mtu hawezi kubatizwa ili hali hajui wala
haamini kwa kile atakachokipokea…. “Aaminiye na kubatizwa ataokoka”
(Mk.16:16)
Hii ni sawa na kusema kuwa mtoto
asijaribu kutembea mpaka awe na uhakika kuwa hatateleza na kuanguka .
Mambo muhimu kabla ya kubatizwa:-
Mtu huanza kwa kulisikia neno la
Mungu; kwa maana Imani huja kwa kusikia.
(Rum 10:17)
Ni lazima kujifunza mambo
unayopaswa kuyafanya ili kuikuza imani yake. Enendeni mkayafnye mataifa yote
kuwa wanafunzi, mkiwabatiza…… na kuwafundisha kuyashika yote niliyoyaamuru mimi. (Mt.28:19,20).
Kasha fanya uamuzi sahihi wa
kumfuata Kristo.
Ni lazima kupata toba na msamaha
wa dhambi. “Tubuni mkabatizwe kila mtu kwa jina lake Yesu Kristo, mpate aondoleo
ya dhambi.” (Mdo.2:38).
Mtu anapotaka kubatizwa ni lazima
atubu ili kupata msamaha wa dhambi zake, na kuyaanza maisha mapya ya kiroho
yenye uwepo wa Mungu, hii ni kwasababu uwepo wa Mungu hutoweka kabisa palipo na dhambi. “Tubuni mkabatizwe kila mtu kwa
jina lake Yesu Kristo, mpate aondoleo ya dhambi.” (Mdo.2:38)
Mtu anapotubu dhambi husamehewa kabisa
na Mungu anasahau kabisa maisha ya awali ya mtu. “Tubuni basi mrejee, ili dhambi
zenu zifutwe.” (Mdo.3:19).
Mtu anapobatizwa mwili wake hugeuka
hekalu la Mungu, yaani huitwa kuunganika kuwa mwili mmoja, “Ndiyo mlivyoitwa katika mwili mmoja”. (Kol.3:15).
Mwili huu mmoja unaozungumziwa ndilo
kanisa, ambapo kichwa chake ni Kristo. “Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha
Kanisa.” (Kol. 1:18)
No comments:
Post a Comment