WAKRISTO NA SIKU ZAO ZA IBADA SURA YA NNE

SURA YA NNE
NIMEKUA NIKIJIULIZA MASWALI MENGI JUU YA UELEWA WA MWANADAMU, ukweli ni kwamba Uelewa wa binadamu ni mdogo sana ukilinganisha na MUNGU BABA.

Mwanadamu amekitoa wapi hiki kiburi cha kupingana waziwazi na MUNGU ile hali ya kuwa Mungu ndiye aliyemuumba..???

Hivi ni nani aliyekuwepo hapo awali kabla ya mwenzie, yaani kati ya Mungu na mwanadamu?
Jibu linapatikana katika kitabu cha Mwanzo 1:1, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. ” Mwanzo 1:28, “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”

Aaah! kumbe mwanadamu aliumbwa na Mungu na siyo binadamu amemuumba Mungu…!
Sasa kwa nini mwanadamu wanatii amri za Mung nusu…..!?
Ama mtu akiongeza wala kupunguza Mungu atamfurahia..!?

Hebu soma nami katika kitabu cha KUMBUKUMBU 4:2, “Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA , Mungu wenu, niwaamuruzo.”
Je maandiko ya Mungu yana faida gani kwa mwanadamu..?

Soma tena nami katika kitabu cha 2 Timotheo 3:16-17 “Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho na kwa kuonya watu makosa yao na kwa kuwaongoza na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”

Pamoja na mafungu hayo machache niliyoyatoa, naomba niitishe kwa kuangalia chuo cha Nabii ISAYA . 22 “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.” 23 “Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.” 24 “Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.” ISAYA 66:22-24.

Sasa ili tuweze kuelewana vizuri ninapozungumzia juu ya ukweli ni lazima mtu kuwa mkweli kwa hali yeyote ile hebu soma yafuatayo;-

Siku zote ukweli ni huu, ukitaka kujua mambo mema siku zote lazima uwe mtu wa kutafakari.
haya mambo ya kubisha pasipo kutafakari ni tatizo.
MASWALI YA KUJIULIZA
1. biblia ni moja kwa nini tunatofautiana, kama siyo uasi ni nini?
2. mambo haya yalikuwepo kabla ya dhambi mfano
   a. NDOA
   b. sabato, yaani siku ya saba baada ya uumbaji.

              Licha ya kwamba leo mambo haya yanaonekana kuwa shida kama kabla ya dhambi yalikuwepo maana yake yalikuwa matakatifu. Fikiria Mungu anaweza kuwewka kitu kisichofaa kabla ya dhambi basi dhambi ilikuwepo kabla ya anguko la Adamu kama Sabato haiona maana. MPENDWA SABATO NDIO ISHARA PEKEE ILIYOWEKWA NA MUNGU KUMTAMBULISHA KWAMBA YEYE NIYE MUUMBAJI NA ALIUMBA KWA SIKU SITA. MUNGU KUONYESHA MSISITIZO AKAAMUA KUIWEKA KATIKA AMRI KUMI.
SIKILIZA INAVYOSEMA AMRI YA NNE

SASA SIKILIZA
1. Ukitunza sabato alafu we ni msengenyaji mbinguni huendi na maanisha kushika sabato hakumpeleki mtu mbinguni.
2. Kuvunja sabato pia kutakufanya kutokwenda mbinguni kwani hujayatimiza mapenzi yote ya Mungu.
3. Nini kitakachomfanya mtu aende mbinguni ni yule aliye moto, si baridi wala vuguvugu na maana ni yeye afanyaye mapenzi yote ya Mungu.BIBLIA  inasema wazi kuwa “mtu ikishi sheria yote ila akajikwaa katika neno moja amekosa juu ya yoye  (Yakobo 2:10) inaama UKISHIKA AMRI ZA TISA ZA MUNGU UKAACHA AMRI YA SABATO UMEKOSA JUU YA ZOTE KUMI.
4. MTU AOKOLEWI KWA KUSHIKA SHERIA/MATENDO BALI ANAOKOLEWA KWA NEEMA NA HII NEEMA INAMFANYA MTU KUBADILI TABIA MAANA YAKE KUANZA KUSHIKA SHERIA mfano mtu ataacha kuzini, kuiba na pia kutunza sabato akirli kuwa Yesu ndiye BWANA na mwokozi wake.

ACHA USHABIKI ELEWA KWA NINI YESU ALITUNZA SABATO HAPO HAPO ALIPINGANA NA MAFARISAYO YESU ALITAKA WAELEWE NAMNA YA KUTUNZA SABATO KWANI SABATO INAAMBATANA NA UPONYAJI HURUMA NA SIYO ANASA ZAKO MWENYEWE NA SHUGHULI ZAKO MWENYEWE.

Utamsikia mwingine anasema ya kwamba MIMI NAONA HAKUNA TABU SANA KILA MTU AENDELEE KUABUDU SEHEMU YAKE. LAKINI NI DAHIRI KWAMBA SABATO MUNGU AKUWAPA WAYAHUDI BALI NI WANA WAISLAELI NDO SISI NDO WW …….KAMA NI HIVYO YESU ASINGEKUWA ANAENDELEA KUABUDU SABATO SOMA LUKA 4:16 NA MITUME WAKE WALIENDELEA KUDUMU KUABUDU SIKU YA SABATO SOMA MATENDO YA MITUME….

 KATIKA KIPINDI CHA DHIKI MATAYO 24:15-24  YESU ANAWAONYA WANAFUNZI WAKE KUWA KUKIMBIA KWAO KUSIWE SIKU YA SABATO……….PIA MIMI NAJUA KUPITIA HATA KATIKA HISTORIA JINSI UFALME WAROMA ULIVYOWATESA WAKIRISTO KIPINDI CHA ZAMA ZA GIZA ZAMA ZA UJINGA (Asomaye na afahamu) KIPINDI HICHO UHURU WA KUABUDU ULITOWEKA KABISA KWANI WATU WALILAZIMISHWA KUABUDU SIKU YA KWANZA YA JUMA …….HAYA NDO MAMBO YANAYOENDELEA TENA HAPA DUNIANI KAMA VILE VITA DHIDI YA NENO LA MUNGU, KUSUJUDIA SANAMU NA MAMBO MENGI MENGI TU.  ILA BIBLIA INASEMA HUYO MNYAMA WA 4 WATU WENGI WATAMSUJUDIA SANA SOMA DANIEL 7 NA UFUNUO12 NA 13 AU LABDA HUYU MUNGU BASI NI KIGEU GEU SOMA ISAYA 66:22- ANASEMAJE?

NILIWAHI KUJIULIZA LABDA BASI WANGEACHA ZILE SIKU ZIJULIKANE KAMA SIKU YA KWANZA YA JUMA HADI YA SABA LABDA WANGEWEZA KUJUA SIKU WANAYOSALI. LAKINI LA! HASHA!! SIKU ZINAJULIKANA VIZURI KABISA KWAMBA JUMAMOSI NI SIKU YA SABA HATA WAO WENYEWE WANAKIRI HIVYO. UKWELI NI KWAMBA SIWEZI KUMFANYIA MTU MAAMUZI YA AIDHA KUSALI  JUMAMOSI AU JUMAPILI AU IJUMAA ILA TUNAWAHUBIRI WATU. IMANI HUJA KWA KUSIKIA

No comments:

Post a Comment