BAADA YA
ANGUKO LA BABELI
Wakaijenga Babeli ikwa mji mkubwa,
watu wote wakiwa na lugha moja. ”Wakasema, haya na tuujenge mji, na mnara,
na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina ili tusipate kutawanyika usoni
pa nchi yote.” (Mwa 11:4)
Baada ya babeli kuanguka, kilamtu
alitoka Babeli akiwa na tamaduni za kipagani kuelekea suhemu mbalimbali za
dunia.”8Basi
BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9Kwa sababu hiyo jina lake
likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipochafua lugha ya dunia yote; na
kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.” (Mwa 11:8,9)
Wakaondoka na ibada zao za kipagani
kilammoja kwa lugha yake wakatawanyika kuelekea sehemu mbalimbali ya uso wa
dunia, ibada ya mama na mtoto ikaendelea kuenea kama desturi yao,
Sanamu ya mama na mtoto ilitambuliwa
kwa majina tofauti tofauti kutokana na kutofautiana kwa lugha. Tamuzi alijulika
kwa majina yafuatayo;-
Huko China, mungu mke alijulikana
kama “Shingmo”
Ufaransa na nchi nyingine za Ulaya
alijulikana kwa majina tofauti tofauti yakionekana kuwa na maana sawa.
Afrodaiti wa
Ugiriki na Venasi wa Kirumi .
Uingereza Tamuzi alijulikana kwa jina
“Ester”.
Neno eostarun katika
Kijerumani ndiko lilikotoka neno la Kijerumani Ostern.
“Asitate” kwa Wagiriki,
“Ashtorethi” kwa Wayahudi.
Huko Efeso mungu mke alijulikana kama “ARTEMI”,
”Kwa maana mmewaleta watu hawa, wasioiba vitu vya hekalu wala kumtukana
mungu mke wetu” (Mdo 19:37).
Ashtorethi
-MALKIA WA MBINGUNI.
Mwanahistoria anayejulikana sana, Will
Durant, katika kazi yake maarufu na yenye kuheshimiwa, Simulizi ya
Ustaarabu, ku. 235, 244-245, ameandika, “Ishita [Asitate kwa Wagiriki,
Ashtorethi kwa Wayahudi], hutuvutia si tu kwa sababu ni sawa na Isisi wa
Kimisri na mfano wa Afrodaiti wa Ugiriki na Venasi wa Kirumi, bali kama mrithi
halali wa moja ya tamaduni ngeni za Kibabeli…anajulikana kwetu hasa kutokana na
ukurasa maarufu katika kitabu cha Herodotus: Kila mwanamke mzawa analazimika,
mara moja katika maisha yake, kukaa katika hekalu la Venasi [Isita], na kufanya
ngono na baadhi ya wageni.”
Je, ni ajabu kwamba Biblia huzungumzia
mfumo wa kidini uliotokana na hilo jiji la kale kama, “SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA
MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI”
(Ufu. 17:5)?
“Watoto
huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili
kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni,
na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.” (Yeremia 7:18)
Mikate
iliyokuwa inatolewa kwa malkia wa mbinguni ilikuwa ni haya haya maandazi ya
moto yenye alama ya msalaba ambayo mamilioni ya watoto leo huimba juu yake
(Alexander Hislop, Babeli Mbili, uk. 107). Kile kinachoonekana kutokuwa
na hatia si safi hata kidogo.
Leo watu wanaweza kufikiri
kwamba wanamwabudu Mwokozi wa kweli wakati kwa hakika wanaabudu mwokozi
bandia—Yesu mwingine! Kwa hakika Ukristo wote wa kawaida unamwabudu Baali,
mpatanishi na mungu jua, aliyeitwa jina kufuatia “mke” wake Ishita (ambaye kwa
hakika alikuwa mama yake Semiramisi)—tutakuja kuona baadaye kuwa ndiye
yule Biblia humwita “Malkia wa Mbinguni.”
“Malkia wa mbinguni” ni nani?
Ashtorethi—Malkia wa Mbinguni
Ibada ya Asitate (Isita) daima
iliambatana na ibada ya Baali au kuabudu jua. Asitate alikuwa mke wa Baali.
Angalia kwamba jina lingine la Asitate lilikuwa ni Ashtorethi. Nukuu ifuatayo
inaliweka hili wazi. “Neno Isita lenyewe lina maana gani? Si jina la Kikristo.
Linabeba asili yake ya Kikaldayo kwenye paji lake la uso. Isita halina
maana nyingine zaidi ya Asitate, moja ya cheo cha Beltisi, malkia wa
mbinguni…Sasa, mungu mke wa Waashuru, au Asitate, anatambulishwa kuwa ni
Semiramisi na Athenagorasi (Legatio, kit. ii. uk. 179), na Lucian (De
Dea Syria, kit. iii. uk. 382)…Sasa, hakuna jina ambalo lingeweza kuonyesha
tabia halisi ya Semiramisi, kama malkia wa Babeli, zaidi ya jina la
‘Asht-tart,’ kwani hilo maana yake ni “Mwanamke aliyejenga minara”…Basi,
Ashturit…ni wazi kwamba ndilo hilo hilo la Kiebrania ‘Ashtorethi’”
(Alexander Hislop, Babeli Mbili, ku. 103, 307-308).
Angalia nukuu hii hitimishi kutoka Ensaiklopidia
ya Microsoft Encarta Multimedia: “Ishita alikuwa Mama Mkuu, mungu mke wa
uzazi na MALKIA WA MBINGUNI.” Hivyo, kiuhakika, Ashtorethi (Ishita) alikuwa
mjane kahaba mama/mke wa Nimrodi, Semiramisi, kama wengi wa wanahistoria wa
kale wanavyoshuhudia! Sasa Isita imewekwa imara kwamba si kitu kingine zaidi ya
Ashtorethi wa Biblia! Sasa tunaweza kuchunguza maandiko yanayoonyesha jinsi
Mungu anavyoitazama ibada ya huyu mungu mke wa kipagani—kwa jina lolote!
Mungu anaichukuliaje Isita?
Sasa kwa kuwa tunajua kuwa Isita ni
mungu mke Ashtorethi, tunahitaji kutazama kwenye Biblia na kuona kile Mungu
anachofikiria. Angalia fungu hili: “Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana...Wakamwacha
Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi [Isita]” (Amz. 2:11, 13).
Muktadha unaonyesha kwamba Mungu
aliruhusu watu Wake wachukuliwe kutoka kwenye
nchi yao kwenda matekani kama matokeo
ya dhambi hii! Huendelea, ikielezea jinsi ambavyo Mungu aliwakomboa watu
Wake mara kwa mara tena kwa njia ya waamuzi. Baada ya kila ukombozi, Israeli
aliwarudia miungu hao hao wa uongo, kitendo ambacho kilileta utekwaji nyara
mara nyingine, kwa kushindwa na mataifa yaliyokuwa yakiwazunguka. Kamwe
hawakuonekana kujifunza kama fungu la 19 linavyoweka wazi. “Lakini ikawa,
wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu… kwa kuifuata
miungu mingine…na…hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi.”
Katika sura ya 10 fungu la 6, Israeli anarudia mtindo huu wa ukaidi. Na Mungu,
vivyo hivyo, bado hukiita kitendo hiki uovu.
Ibada za Baali na Ashtorethi
zilijitokeza wakati wa Samweli. Samweli aliwaambia Israeli, “…iondoleeni
mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee Bwana
mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake...Ndipo wana wa Israeli wakayaondoa
Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia Bwana peke yake” (1 Sam. 7:3-4).
Baadaye, katika 1 Samweli 12:10-11, Samweli aliielezea historia ya Israeli
hadharani. Aliwakumbusha kwamba waliendelea kurejea katika kumtii Mungu, kisha
kurudia ibada ya sanamu tena na tena!
Imesemwa kwamba “Kitu pekee ambacho
mwanadamu amejifunza kutokana na historia ni kwamba hakuna mtu anayejifunza
kutokana na historia.” George Santayana alienda mbele zaidi na kusema, “Wale
wasiojifunza funzo la historia wana hatari ya kuirudia.”
Somo hili linawaelezea Israeli wa
kale—lakini pia linaelezea ulimwengu mpya wa leo. Kwa sababu Isareli hawakudumu
katika njia, hatimaye walitekwa mateka, wakapotea kutoka katika historia! Baada
ya kutekwa nyara na kuadhibiwa mara moja zaidi, unabii unafunua kwamba Kristo
atawakusanya kwa mara ya mwisho wakati wa Kurudi Kwake.
Mfano mwingine kutoka kwenye biblia.
Biblia husema kuwa Mfalme Sulemani
alikuwa ndiye mtu mwenye hekima sana aliyewahi kuishi. Bado, alifanya kosa
ambalo Mungu aliliona ni kubwa sana kiasi kwamba, baada ya kifo chake,
Alimwadhibu Sulemani kwa kuuondoa ufalme kutoka kwa mtoto wake.
Kosa lake?
Alioa mwanamke aliyemwongoza katika
kumwabudu Isita (Ashtorethi).
Angalia 1 Wafalme 11:4-6: “Maana
ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu
mingine...Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa
Wasidoni…Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata
Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.” Mafungu ya 11-12
yanaonyesha kwamba ufalme ulichukuliwa kutoka kwa mtoto wake.
Ibada ya sanamu ikiwemo desturi yao
ya sala za kujirudiarudia ilisambaa na kuenea duniani kote, mfano mzuri was ala
na namna hii zinaonekana huko Efeso. “Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni
myahudi, wakapiga kelele wote kwa pamoja kwa muda wa kama saa mbili wakisema,
Artemi wa Waefeso ni mkuu” (Mdo 19:34).
Mfumo huu wa sala ya kujurudiarudia
ulionekana kushamiri sehemu mbalimbali katika uso wa dunia. Sheria kali
ziliwekwa kwaajili ya mtu yeyote atakayepinga na kuidharau miungu yao.
Wakati mtume Paulo aliokua Assia
akihubiri neon la Mungu walimshtaki na kumouna kuwa ni mtu anayekiuka maadili
na kumdharau mungu wao mke Artemi. “Tena mnaona na kusikia ya kuwa si katika
Efeso tu, bali katika Asia yote, Paulo huyo ameshawishi watu………. Si kwamba kazi
hii yetu ina hatari ya kudharauliwa tu; bali hekalu la mungu mke aliye mkuu,
Artemi , kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambaye Asia yote pia
ulimwengu wote humwabudu” Mdo(19:26).
Hili “kanisa mama” lina “mabinti madhehebu” wengi, na mfumo
mzima hujificha chini ya bendera ya “Ukristo”, wakati kwa hakika ni “Dini ya
Kisiri ya Kibabeli.” Biblia humwonyesha kama mdanganyifu wa watu wote pamoja na
nchi zote za Kikristo zikiwa zimeleweshwa na mafundisho yake ya uongo!
Anaonyeshwa kama aliyelewa kwa damu ya watakatifu, wakati huo huo, akijidai
kwamba yeye ndiye kanisa la kweli. Mambinti zake wote wamerithi matendo yake ya
kipagani.
Mamia ya mamilioni hutunza sikukuu ya ibada halisi ya miungu
ya kipagani inayoitwa Isita, wakiamini kwamba wanamwadhimisha Yesu Kristo!
Wengi hawajui kabisa kuhusu nini wanachokifanya. Jibu la Mungu kwa wote hawa ni
“…zamani zile za ujinga Mungu alijifanya
kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu”
(Matendo 17:30)!
Lakini hebu tuone Yesu mwenewe anasemaje, Yesu aliwaambia
Mafarisayo,“Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu. Nao waniabudu bure, Wakifundisha
mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu”
(Math. 15:6, 9).
Maelezo sambamba ya Marko huongezea kitu cha muhimu:
“Vema! Mwaikataa amri ya
Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu”
(Mk. 7:9).
Kwa
wazi mafungu haya yanawahusu wale wanaoikataa Pasaka ili wapate kutunza Isita
ya kipagani.
No comments:
Post a Comment