BAADA YA
GARIKA
NURU aliishi miaka miatisa na hamsini
kasha akafa. “siku zote za Nuru zilikua miaka mia kenda na hamsini, akafa. (Mwa 9:29)”. Mpango wa shetani wa kuendelea
kuwapoteza wana wa Mungu uliendelea.
Vizazi vya wana wa Nuru vilizidi
kuzaliana na kuongezeka kadiri siku zilivyokua zikipita. Vilipita yamkini
vizazi kadha wa kadha kasha akazaliwa NIMRODI ambaye ndiye tutamzungumzia
katika sura hii.”1Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuru, Shemu
na Hamu na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. 2Wana
wa Yafethi ni………… 8Kushi
akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi” (Mwa. 10:1-8)
NIMRODI alikua mtu aliye jaliwa
uhodari wa kupambana na wanyama pori hasa kipindi kile baada ya gharika ambapo
walikua wakisumbuliwa na wanyamapori.
Kwakua unabii ulikua unaeleza wazi
kuwa atazaliwa MASIHI kwa njia ya wanamke, na kwa njia hiyo ulimwengu wote
utaokulewa kupitia kwake, shetani aliamua kuwapotosha watu wa Mungu juu ya
mpango mzima wa kuzaliwa kwa MWOKOZI.
Baada ya gharika watu walianza kuhama
na kuelekea upande wa mashariki nyanda za chini kuliko na tambarare. Ukanda huu
ndi ulikua na ardhi nzuri yenye rutuba iliyokuwa ya udongo wa tifutifu. Udongo
huu ulizolewa kutoka sehemu mbalimbali na maji ya Gharika kutoka nyanda za juu.
Watu walianza kuhama na kuelekea
katika eneo hili lenye rutuba ili kulima nafaka. Na huko ndiko nchi ya Shinari
ilikojengwa.” Mwanzo wa ufalme wake ulikua Babeli na Ereku, na Akadi, na Kane,
katika nchi ya Shinari” (Mwa
10:10).
Shinari ni nchi iliyokua imejaa na
kufunikwa na misitu minene, kutokana na udongo wake wenye rutuba hivyo walikua
wakishambuliwa mara kwa mara na wanyama pori hatari kama vile Simba, Chui na
wanyama wengine.
Ndipo walipotafuta msaada wa mtu
yeyote ambaye angeweza kuwaondolea tatizo hilo la kuvamiwa na wanyama pori, na
kuahidi kuwa iwapo angepatikana mtu ambaye angewaondolea tatizo lile wangempa
heshima kuu.
Alikuwepo mtu mmoja,NIMRODI ambaye
alikua hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana, Biblia inamtambua.” 8Kushi
akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi 9Alikua hodari
wa kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwahiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hidari wa
kuwinda wanyama mbele za BWANA”(Mwa 10:8,9)
Ndipo walipo msihi sana Nirodi
awasaidie kuwaondolea tatizo lile. Nimrodi alifaikiwa kupambana na wale wanyama
hatari ka kufanikiwa kulipunguza na kuliondoa tatizo lile. Kwakua tatizo lile
lingeweza kurudi tena mda wowote, Nimrodi aliwasihi kujenga mji na kujenga
ukuta kuzunguka mji wote. Hivyo ndivyo wangeweza kuwa salama zaidi.
Walifanikiwa kuujenga mji na kujenga
ukuta kuzunguka mji wote. Mji huo ukaitwa “MJI WA BABELI”. Kutokana na desturi
ya watu wa kale walihitaji kupata mtawala “MFALME” ambaye angewaongeza. Kwa
heshima kuu walimsihi Mimrodi awe mfalm wao.
Nimrodi akawa mfale wa kwanza Wa
BABELI, na ndiye mfalme wa kwanza kutajwa katika Biblia kuongoza watu baada ya
GHARIKA, Biblia inamtambua. .” Mwanzo wa ufalme wake ulikua Babeli na
Ereku, na Akadi, na Kane, katika nchi ya Shinari” (Mwa 10:10).
Hebu turejee vitabu vya kihistoria na
maandiko kutoka kwenye biblia,
Mke
wa Nimrodi
Jina
la Bibi wa Nimrodi ni Ishtar ama Easter. Bibilia yamtaja kama Ashtoreth.
Watu wengi walimwita Semiramis na Frazer, (The Golden Bough, ii 275). Njia za hila zake kufanywa kusini
mwa Uganda. Jina lingine la Semiramis ni Phrygian Cybele na Assuru
Atargati. Jina Atargati ni la kiyunani, kusema Baali ya Tarsus, huko sasani
Assuru. Jina lake zamani ilikuwa Atheh-Atheh kumaenisha Mungu mwanamke wa
Tarsusi. Mafundisho yake ya uongo ilienea mpaka kaskazini mwa Hieropolis
Bambyce karibu na mto Frati (Frazer ibid.
v, 162 and n 2,3).
Bwana
wake alipokufa, bibi alinyakua mamlaka na kwa sababu watu wengi walikuwa
wamepoteza matumaini ya Nimrodi kuwa kama Mungu, kama alivyosema. Seminari
aliogopa kupoteza mamlaka yake, na akatafakari hila ya kuondoa ili
wamkubali. Hila ya kuwashtua na miuliza ya kufanya waamini kweli Nimrodi
alikuwa Mungu.
|
Baadaye
semiramisi akapata mtoto wa kiume, Hii ilikuwa njama na hila ya kudanganya
wafuasi wake. Alieneza uvumi ya kwamba mtoto hakuwa na baba, lakini
alizaliwa kwa mimjiza kutokana na miale ya jua. Alifahamika kama mtoto wa
kurithi ufalme wa Nimrodi.
Huu
undanganyifu ulikuwa wa hali ya juu wa kuamini, lakini seminari alifaulu
kutawala ufalme. Nimrodi alionekana sana kama motto wa Mungu. Na kwa ajiri
ya juhudi zake za undanganyifu seminari aliabudiwa kama ndiye mama wa
Mungu. Alijuukana kama “Mama Bikira” au malkia wa mbinguni (Jer 7:18, 44:17-19,25).
Ni yeye mama wa kwanza kuwa wa dini ya uongo. Mafundisho ya uongo
yaliyomfuata ni ya “Cybele ka mama Mungu huko kati ya mashariki.
Haya yote
yametendeka zaidi ya miaka elfu nne iliyopita. Ulikuwa mwanzo wa kuabudu
sanamu na imekuwa na uwezo kwa karne nyingi zilizopita, hata siku ya leo,
watu wengi wanamwabudu “Malkia wa mbignuni” hata ingawa hakuna mtu kama
huyo.
|
Mfalme Nimrodi akamuoa mke
aliyejulikana kwa jina Shemiramisi. Shemiramisi kama malkia wa nchi ile aliishi
mdamrefu na mumewe mfalme Nimrodi bila kupata mtoto. Baada ya miaka michache
Nimrodi alikufa. Watu wote wa mji ule wa Babeli walihuzunishwa san ana kifo cha
mfalme wao NIMRODI.
Baada ya miaka kadhaa kupita, malkia
Shemiramisi alipata ujauzito, watu wote walishangaa ni kwa jinsi gani malkia
aliweza kuishi na Mfalme Nimrodi bila kupata mtoto. Ili kuficha aibu na
kutokuonekana mzinzi, yeye mwenyewe alidai alipata ujauzito kwa njia isiyokua
ya kawaida, (KWA NJIA YA MIONZI YA JUA).
Malkia alidai kuwa mfalme Nimrodi
alienda kwa Mungu jua na kwa kuwa watu Babeli wanateseka, mfalme nimrodi
ameamua kurudi tena kuja kuwaokoa watu wake.
Ghafla ibada za kibabeli zikaanza
kufanyika kwa kuangalia jua. Wanadamu walizidi kumchikiza Mungu kwa kufanya
mambo ambayo waliyaona ndiyo IBADA ya kweli. “8Akanileta mpaka ua
wa ndani ya nyumba ya BWANA, na tazama, mlangoni pa hekalu la BWANA, kati ya
ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo
hekalu la BWANA, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu
jua” (Eze 8:16).
Mungu
ametuonya kupokea mila za wale wanaoabudu sanamu (Kum. 12:30-31) Viongozi wengi
wa kanisa wanatuambia ni ushenzi kutoshika na kuheshimu 25 Decemba kama
sikukuu. Hii siku ilisherekewa na washenzi kwa ajili ya kuzaliwa kwa mtoto na
malkia wa mbinguni aliyehusishwa na Nimrodi kama Mungu wa jua.
Wafuasi
wake wakasema kwa kua tarehe 25th Decemba mti ulinenepa kwa siku
moja huko Babeli na Nimrodi angerudi kwa siri tarehe hiyo kila mwaka kuacha
zawadi kwa huo mti, aliteremka kama yai kubwa kutoka mbinguni na kuanguka mto
frati. Mungu aliyekuja kama yai, si mwingine bali ni ISHTAR. Huo ndio ni mwanzo
wa krismasi, Soma karatasi “Kwa nini tusisherehekee krismasi. Why we don’t
celebrate Christmas (No. CB24).
Baadaye malkia akaza mtoto akamwita
jina lake TAMUZI, Tamuzi alizaliwa tarehe 25 ya mwezi wa kumi na mbili, ambapo
siku hiyo kwa heshima ilifanywa ni siku ya amani na msamaha wa wafungwa
ulitolewa siku hiyo Biblia inalieleza hilo. “31Hata ikawa, katika
mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake mfalme Yehoyakini, mfalme wa
Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi,
Evil-merodaki, mfalme wa Babeli , katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake,
akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani.” (Yeremia 52:31)
Tamuzi alionekana kama mkombozi wao
aliyeletwa na Mungu mwenyewe. Uongo dhidi ya ukweli juu ya mpango wa ukombozi
wa Ulimwengu kwa njia ya Mwokozi atakayezaliwa na mwanamke ulionekana kama
umukwishatimia.
Ghafla ALAMA ZA MOTO kama vile
mishumaa ZIKAANZA KUWEKWA KATIKA NYUMBA ZA IBADA ili KULIENZI JUA(mungu jua) katika siku
ambazo jua halijachomoza.
Shemiramisi hakutaka tu aheshimiwe
mtoto peke yake, bali pia mama. Baada ya miaka michache kupita mtoto Tamuzi
alikufa. Watu wote walisikitishwa sana na kifo cha mungu mtoto TAMUZI.
Watu waliendelea kufanya mambo ambayo
yalimchukiza Mungu kama nabii Ezekiel anavyoeleza. ”Akaniambia, mwanadamu, umeyaona
haya? Utaona tena machukizo makubwa kuliko hayo.” (Eze 8:15)
Baada ya kifo chake Tamuzi, sanamu za
kumuenze Tamuzi zikasimamishwa katika nyumba za ibada, Biblia inaeleza. “Ndipo
akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya BWANA, ulioelekea upande
wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi”(Eze 8:14)
Tamuzi alikufa katikati ya mwishoni
mwa mwezi wa tatu na mwanzonimwa mwezi
wa nne. Baada ya miaka kadhaa kupita malkia shemiramisi naye akafa. Ibada ya
mama na mtoto ikaanza kushamiri katika Babeli na Yuda yote. Malkia Shemiramisi
kwa hishima akapewa jina la MALKIA WA MBINGUNI.
Ghafla sanamu za ibada ya mama na
mtoto zikasimamishwa katika nyumba za ibada. Sanamu hizo zilikua sanamu ya MAMA(Shemiramisi)
AKIWA AMEMBEBA MTOTO MIKONONI MWAKE(Tamuzi). Sanamu hizi zilikua zikipewa
heshima kubwa katika nyumba za ibada, mashirika mbalimbali ya kinamama
yaliundwa na kuamriwa kuamfukuzia uvumba ile sanamu ya malkia wa mbinguni, na
kuitunza.
Wakasahau na kuihalifu sheria ya
Mungu iliyo kataza sanamu, “1Msifanye sanamu yo yote, wala
msijisimamishie sanamu a kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote
lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu
wenu” (Kut 26:1)
Kinamama walikua wakiamriwa na
waumezao kujiunga katika mashirika na kuiabudu ili sanamu, Biblia inaeleza. “17Lakini
bilashaka tutalitimiza kilaneno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukuzia
uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotena
sisi na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji wa Yuda…………….
Maana wakati huo tulikua na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya” (Yer 44:17)
Imani zao zilikua kwa miungu na
walipoacha kuiabudu, walipatwa na majanga, pomoja na kupungukiwa na chakula. “Lakini
tulipoacha kumfukuzia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za
vinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga na kwa njaa.” (Yer 44:18)
Kila mume alihakikisha kuwa mke wake
amejiunga na shirika ili kuziabudu sanamu zao, na uziunza, Biblia inaeleza
vizuri sana.”Nasi tulipomfukuzia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka
za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko,
waume zetu wasipokuwepo?” (Yer 44:19)
No comments:
Post a Comment