UNABII KUHUSU BABELI NA HATIMA YAKE
Katika enzi ya manabii wa Israeli (Kama 850-560 K.K)
kuliinukia dola mbili kuu katika maeneo yanayoizunguka mito ya Frati na
Tigrisi, katika Iraki ya sasa. Ya kwanza ilikuwa dola ya Ashuru iliyokuwa na
makao makuu Ninawi.
Kwa karne mbili, Waashuru walivamia ardhi ya mataifa waliowazunguka: kusini
wakawatawala Wakaldayo na makao makuu yake Babeli; na kupitia Israeli mpaka
Misri. Sera yao ilikuwa kuwatishawakazi wa maeneo hayo watii na kulipa kodi kwa
mwaka. Kufanikisha hili waliiswaga miji kiuporaji na kuichoma moto, wakavibamiza
vijiji, na kuua wakazi na kuchukua maelfu ya mateka Ashuru.
Katika nusu ya pili ya karne ya saba (K.K), nguvu ya Ashuru
ilipungua na Babeli ikaanza kupanda. Katika mwaka 612 (K.K), Ninawi uliangushwa. Nebukadreza,
mfalme wa Wakaldayo, haraka akaanzisha dola mpya.
Mataifa madogo madogo Mashariki ya Kati yalipokuwa
yanashangilia uhuru wao kutoka Ashuru, mara yakajikuta wakivamiwa na majeshi ya
Babeli. Nebukadreza akaivami Israeli akaiteka Yerusalemu, akalichoma
hekalu lake na kuchukua maelfu ya mateka
Babeli.
Dola ya Babeli ilikuwa ni
awamu ya pili ya utawala huu wa kijeshi. Ulikuwa katika eneo la Frati.
Nebukadreza, aliujenga mji mkuu wa Babeli kuwa fahari ya dunia. Alijenga
Mahekalu makubwa na majumba ya kifalme, na kuzungushia jiji hilo ukuta mkubwa sana
kuulinda. Babeli ukawa utukufu na fahari kuu kwa Nebukadreza mwenyewe na
Wakaldayo wake.
MAANGUKO KAMILI
Miaka 100 kabla Babeli haijafikia kilele cha ukuu wake, nabii
Isaya alishatabiria kuangushwa kwake kwa maneno thabiti sana. “…Siku
ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi
Mungu…Tazama, nitawaamsha Wamedi juu yao…Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa
kama Sodoma na Gomora hapo Mungu
alipoiangamiza. Hautakaliwa na watu tena kabisa… Lakini huko watalala hayawani
wakali wa nyikani” (Isaya
13:6,17,19-21).
Nabii mwingine, Yeremia, akiandika miaka 100 baadaye, wakati
Nebukadreza alipokuwa akikaribia kuivamia Yerusalemu, aliongeza mtazamo juu ya
anguko la Babeli. Na mwishowe nabii anaamriwa kufunga jiwe kwenye gombo la
unabii ule na kulitupia ndani ya mto Frati, aseme, “Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli,
wala hautazuka tena…”
Soma kifungu cha (Yer:51:1,8,28,37,58,62-64).
Historia inaonyesha jinsi ambavyo unabii huo wa maanguko ya
Babeli ulivyotimizwa hatua kwa hatua. Wavunjaji
wa Kwanza walikuwa Wamedi na
Wajemi katika karne ya sita (K.K). Baadaye walikuja Wayunani chini ya
Aleksanda Mkuu, wakifuatiwa na Warumi; baada yao makabila kadhaa yapendayo vita
kama Wapathi, Waarabu na Watarta.
Kwa karne nyingi mahali halisi pa jiji la Kale la Babeli
palikuwa mahame, yaliyoepukwa -wasafiri wasemavyo -na wahamaji wanaotangatanga. Ni hivi karibuni tu
wataalamu wa kihistoria wachimbuao chini (Archaeologists), walipochunguza eneo
hilo katika nusu ya kwanza ya karne ya 19, na kugundua mabaki ya kuta kubwa,
mahekalu ya nguvu na malango, na
masanamu makubwa yaliyoonyesha ulimwengu ulioshikwa na butwaa jinsi ukuu wa
Babeli ulivyokuwa enzi zake.
Kwa hiyo historia inatuonyesha jinsi Babeli ‘Utukufu wa
falme,’ ulivyoangushwa na kuachwa, kama manabii wa Israeli walivyotabiri
ingekuwa.
Nani angeweza kujua?
Utabiri wa mambo wa muda mrefu hivyo unawezekanaje? Kuna jibu
moja tu linaloridhisha; Lazima awep aliyeyajua kabla; lakini ni nani? Kwa
hakika hakuna mtu wa miaka 2500 iliyopita au tangu hapo, angeweza kujua.
Tukiupima utabiri wa namna hii kibinadamu tu hauelezeki.
Lakini hata hivyo, manabii wa Agano la Kale hawakudai wanatabiri kwa uwezo wao.
Walisema walikuwa wakisema manena yaliyotoka
kwa Mungu. “ Hivi ndivyo asemavyo BWANA,” ndivyo walivyokuwa wakianza
kusema wakati wote.
Kama Mungu alikuwa nyuma ya yale waliyosema,
tunapata jibu la nani aliyejua.’ Hakuna maelezo mengine yanayoleta maana.
Unabii tuliouchunguza hapa ulihitaji uwepo wa Mungu kama chanzo chake
No comments:
Post a Comment