VITA
KWA NJIA YA MAOMBI
"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;
bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya
pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" EFE 6:12.
Ndugu
yangu, Paulo anatueleza jambo zito sana katika waraka wake huu. Paulo
anatufundisha kubeba silaha zote za kupigana na adui ili tuweze kusimama kwa
ushindi katika hivi vita. Pamoja na silaha zote anamalizia katika mstari wa
kumi na nane kwa kusema kwamba "kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho,
mkikesha kwa jambo hilo ".!
Anatuambia
kwamba kupigana kwetu huku ni kwa njia ya maombi! Kimahesabu, vita vyetu hivi
tunavipiga kwa kutumia maombi. Vita hivi vya kiroho tunavipiga kwa kutumia
maombi. Maombi ni silaha kubwa katika vita hivi. Ukiangalia silaha zote ambazo
anazitaja
1. Kweli
2. Haki (Maisha safi yenye
utii)
3. Utayari ktk huduma
4. Imani
5. Wokovu (Uhakika wa
mahusiano ya mtu binafsi na Mungu)
6. Upanga wa Roho ambao
Neno la Mungu.
Silaha
kuu yenye kubeba silaha zote hivi ni maombi! "kwa sala zote na maombi
mkisali kila wakati katika Roho".
Ndugu,
kila siku unapaswa kukaa mkao wa kivita. Paulo anamuonyesha adui kama mtaalamu
wa kupanga vita hivi. Ndo maana Paulo asema ktk mstari wa kumi na moja "Vaeni silaha
zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani". Shetani
ni mwenye hila kila wakati. Katika kazi zako ataweka hila, katika huduma yako
ataweka hila. Katika kanisa lako ataweka hila. Katika uchumi wako ataweka hila.
Kila kutaka kwako kumjua Mungu ataweka hila. Basi Paulo asema Vaeni silaha zote
za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Basi acha kulala mtumishi.
Simama tuvipige hivi vita. Kuna watu wanajiona hawana huduma katika kanisa.
Huduma hii ya ukamanda wa maombi nafasi hii inakusubiri. Mavuno ni mengi,
lakini watenda kazi ni wachache. Chukua hatua. Tumia mbinu zote za kivita vya
kiroho tuweze kupambana na adui.
Tuungane
pamoja katika vita hii pia kwa ku-like page yetu tushirikiane katika kuvipiga
vita hivi katika jina la Yesu na damu ya mwanakondoo.