Tuesday, March 29, 2016

HATIMAYE SIKU ZA IBADA KUBADILIKA

BADILIKO KATIKA UTUNZAJI WA SIKU YA SABA
 Mahali fulani katika zama za giza katikati ya siku zile za Kristo na siku zetu, utunzaji wa Sabato umebadilishwa kutoka siku ya saba ya juma kwenda siku ya kwanza.
Ni hakika ya kwamba amri ya Mungu inahusu kuitakasa na kuitunza siku ya saba kama Sabato. Hakuna uwezekano wowote wa kukosa kuelewa maana yake hapa. Amri ni hii:
"Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa." (Kutoka 20:8-11). .....Soma Zaidi.

No comments:

Post a Comment